Mtumiaji:Tumaini Mwenda Ruleju
Mandhari
Bioteknolojia ya kilimo
[hariri | hariri chanzo]Bioteknolojia ya kilimo ni nyanja ya sayansi ya kilimo inayohusisha matumizi ya zana na mbinu za kisayansi ikiwemo uhandisi wa vinasaba, viashiria vya molekuli, uchunguzi wa kijenetiki na chanjo kwa ajili ya kuboresha viumbe hai: mimea, wanyama na vijidudu.
Bioteknolojia ya mazao ni sehemu mojawapo ya bioteknolojia ya kilimo ambayo imeendelea sana katika siku za hivi karibuni. Sifa zinazohitajika huhamishwa kutoka spishi fulani ya zao hadi spishi nyingine. Mazao haya ya transjeni huonyesha sifa zilizoboreshwa mfano: ladha, rangi ya maua, kasi ya ukuaji, ukubwa wa mazao yanayovunwa, na uwezo wa kuhimili magonjwa pamoja na wadudu.