Mtumiaji:Suleiman Mtokambali
Suleiman Mtokambali
[hariri | hariri chanzo]| Suleiman Mtokambali | |
|---|---|
| Makazi | Dodoma, Tanzania |
Suleiman Mtokambali (amezaliwa 3 Desemba 1993) ni mchumi kutoka Tanzania. Amewahi kufanya kazi katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na utafiti wa mabadiliko ya bei za mazao ya kilimo. Kwa sasa anaishi jijini Dodoma pamoja na familia yake.
Maisha ya Awali na Elimu ya Msingi
[hariri | hariri chanzo]Suleiman alizaliwa katika Hospitali ya Wahindi ya Shree Hindumandal iliyopo Posta, Dar es Salaam. Wazazi wake ni Ostack P. Mtokambali na Sebastiana E. Haule. Familia yao ilianza maisha katika eneo la Manzese kabla ya kuhamia Ubungo Riverside. Mnamo mwaka 1996, walihamia Tabata Kisukuru baada ya kukamilika kwa ujenzi wa nyumba yao ya kwanza.
Mwaka huohuo, wazazi wake walitengana. Baba yake alielekea kusoma katika Chuo Kikuu huku mama yake akirejea Ludewa, Mkoa wa Njombe, akiwa na Suleiman. Akiwa huko, alilelewa na mama pamoja na babu na bibi zake. Alibatizwa katika dhehebu la Kanisa Katoliki na kuanza masomo ya awali katika Shule ya Msingi Lufumbu.
Mnamo mwaka 1999, Suleiman alirejea Dar es Salaam na kuendelea na masomo yake katika shule za msingi Kisukuru na Jeshini Kibangu. Mwaka 2001 hadi 2005, aliendelea na masomo katika Shule ya Msingi Segerea kabla ya kuhamia Shule ya Msingi Ujamaa, Kibena, Njombe kutokana na changamoto za kifamilia.
Elimu ya Sekondari
[hariri | hariri chanzo]Kuanzia mwaka 2008 hadi 2011, Suleiman alisoma katika Shule ya Sekondari ya Wende, Njombe. Alikumbana na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na tuhuma za uongo zilizompelekea kuadhibiwa. Tukio hili lilimfanya kurejea katika imani ya Kanisa Katoliki na kujiunga na kwaya.
Mwaka 2009, aliteuliwa kuwa kiongozi wa darasa na baadaye kuwa Mkuu wa Taaluma (Academic Prefect). Alionyesha umahiri katika masomo ya Biolojia, Hisabati, Uraia na Fizikia, akitunukiwa vyeti vya ufaulu na zawadi maalum mwaka 2011 alipohitimu.
Kidato cha Tano na Sita
[hariri | hariri chanzo]Kuanzia mwaka 2012 hadi 2014, Suleiman alisoma katika Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Matayo (St. Matthews High School), Mkuranga. Alisomea masomo ya Jiografia, Uchumi, na Hisabati (EGM). Aling’ara katika masomo hayo hasa Jiografia, japokuwa hakupata tuzo rasmi kutokana na tuhuma za upendeleo.
Elimu ya Juu
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Oktoba 2014, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) akichukua Shahada ya Uchumi na Takwimu (BAEST). Licha ya kutopata mkopo, alihitimu mwaka 2017 kwa msaada wa baba yake.
Baada ya kuhitimu, alijishughulisha na biashara ndogo ndogo na kazi mbalimbali ikiwemo ujenzi na uendeshaji wa stationery hadi mwaka 2019. Alijaribu pia shughuli za kilimo vijijini Njombe na Ruvuma.
Mnamo Julai 2019, alipata ajira kama mchumi mjini Dodoma. Mwaka 2021 alianzisha familia na kujiunga na masomo ya uzamili ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), akitunukiwa shahada ya Uzamili (MA in Economics) mwezi Novemba 2024.
Maisha Binafsi
[hariri | hariri chanzo]Suleiman ameoa na ana watoto kadhaa. Kwa upande wa familia, yeye ni mtoto wa pili kwa baba yake, akiwa na kaka mmoja (Seleman Mtokambali) na dada mmoja mdogo (Regina Mtokambali). Kwa mama yake, yeye ni mtoto wa kwanza na ana wadogo wawili: Anastazia Haule na Emilia Mligo.
- ↑ Mbijima, Rose Jackson (2024-06-30). "Uhakiki wa Kimwingilianomatini katika Fasihi ya Watoto: Mambo ya Msingi ya Kuzingatia". MULIKA. 43 (1): 136–154. doi:10.56279/mulika.na43t1.8. ISSN 0856-0129.
- ↑ "Home | University of Dar es Salaam". www.udsm.ac.tz. Iliwekwa mnamo 2025-04-25.