Mtumiaji:Tsavo Mashariki
Tsavo Mashariki
[hariri | hariri chanzo]HISTORIA
[hariri | hariri chanzo]Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki ilianzishwa April 1948[1]. Tsavo Mashariki ina ukubwa wa kilomita za mraba 13,000 na iko katika eneo la kusini mashariki mwa Kenya. Tsavo Mashariki ilianza kama kimbilio la wanyamapori. Kulikuwa na tembo elfu arobaini na tano, na vifaru elfu nane. Watu walioenda Tsavo Mashariki waliishi katika ardhi. Hapakuwa na nafasi ya kutosha kwa tembo. Watu waliwinda tembo kutafuta pembe. Tembo wengi walikufa kwa sababu ya uwindaji. Tsavo Mashariki iko katika Kaunti ya Taita-Taveta.
Hifadhi ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki ni muhimu kwa hatua za awali za uhifadhi wa wanyamapori nchini Kenya. Kuanzishwa kwa mbuga hiyo ilikuwa sehemu ya harakati pana za kuhifadhi wanyamapori na mazingira asilia ya Kenya. Katika mwaka wa 1990, Tsavo Mashariki iliboresha sheria za kupambana na ujangili, na kuongeza ufadhili kwa usimamizi wa mbuga, kusaidia kulinda idadi ya wanyamapori katika mbuga hiyo.
Waswahili walifanya biashara na wakaaji wa Tsavo walifanya biashara ya pembe za ndovu, ngozi za paka, na pengine watumwa mapema kama mwaka wa 700 CE. Wavumbuzi wa karne ya 19 Waingereza na Wajerumani waliandika kuhusu watu wakati wa safari zao mbugani. Simba wanaofahamika kama Tsavo Man-Eaters walitishia wasafiri nchini Kenya. Wavumbuzi waliwaua simba hao baada ya simba hao kuwaua Wahindi mia moja thelathini na tano na wafanyakazi wa ndani.
WANYAMA
[hariri | hariri chanzo]Kuna wanyama wengi katika Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki. Hifadhi ya Taifa ya Tsavo Mashariki ina “wakubwa watano” wanyama. Kuna tembo, simba, chui, nyati, na kifaru. Watu huwaita wanyama hao “wakubwa watano” kwa sababu ndio wanaotafutwa sana kuwaona safarini. Tsavo Mashariki ina idadi kubwa ya tembo nchini Kenya. Kuna tembo zaidi ya elfu kumi na mbili katika hifadhi hiyo. Tembo hao wanaonekana katika makundi makubwa karibu na Mto Galana na Bwawa la Aruba. Tsavo Mashariki ina simba wasio na manyoya ya shingoni (manes). Simba hawa ni maarufu. Wao ni wa kipekee kwa sababu madume wana manyoya mafupi au hawana kabisa. Chui ni nadra kuona katika Hifadhi ya Tsavo Mashariki. Nyati ni hatarishi katika Hifadhi ya Tsavo Mashariki kwa sababu wanaweza kuambukiza magonjwa kwa wanyama wengine. Vifaru wako hatarini kutoweka kwa sababu wanawindwa. Wanawindwa kwa sababu ya pembe zao. Duma katika Hifadhi ya Tsavo Mashariki wanawinda paa. Unaweza kuona duma mchana, lakini huwezi kuona usiku. Twiga ni wa kawaida katika Hifadhi ya Tsavo Mashariki kwa sababu wanapenda miti ya acacia. Pundamilia wanaweza kuonekana katika makundi. Wanapenda kula majani. Viboko wanaweza kuonekana karibu na mito kwa sababu wanapenda maji. Wanapenda kufuga. Viboko wanaweza kuonekana karibu na mito kwa sababu wanapenda maji.
MITI NA MAUA
[hariri | hariri chanzo]Maua maarufu zaidi katika Hifadhi ya Tsavo Mashariki ni maua ya “White Morning Glory”. Yanajulikana sana kwa kufunika tambarare kubwa baada ya mvua. Pia kuna maua mengi ya zambarau na bluu. Miti inayojulikana zaidi ni miti ya mininga. Ina vifuniko vya juu vya gorofa ambavyo hutoa kivuli. Miti ya mibuyu pia ni ya kawaida. Ina mashina makubwa sana. Inaitwa “mti wa uzima.” Miti na maua ni muhimu sana kwa mazingira ya Tsavo Mashariki. Zaidi ya spishi 500 za ndege zimeonekana katika eneo hilo.
VITISHO
[hariri | hariri chanzo]Uwindaji haramu wa tembo ni tatizo kubwa katika Hifadhi ya Tsavo Mashariki. Pembe za ndovu kutoka kwa mikonga ya tembo ni za thamani. Serikali inajaribu kukomesha ujangili. Tembo wawili wakubwa waliouawa hivi majuzi katika Hifadhi ya Tsavo Mashariki. Watu ambao serikali ilifikiri kuhusika katika uwindaji haramu huo walikamatwa.
Tishio lingine ni ukame. Ukame ni mbaya kwa Tsavo Mashariki kwa sababu wanyama hutegemea maji. Ukame ni mbaya kwa mazingira pia kwa sababu maua yanahitaji maji ili kuishi vizuri.
- ↑ "Tsavo East National Park", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2025-10-28, iliwekwa mnamo 2025-12-12