Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Sikudhani Yahaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

UTANGULIZI: Sikudhani Yahaya Damian, jinsia (me) nilizaliwa tarehe 24/04/1986 katika mtaa wa Kalangala Wilaya ya Geita na Mkoa wa Mwanza, ni mtoto wa kwanza katika familia yenye watoto wawili, kabila langu ni Msukuma, elimu yangu ya awali nilisoma katika shule ya msingi ikulwa iliyoko wilayani Geita mwaka 1994 hadi 2001 nilichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule ya sekondari kalangala wilayani Geita mwaka 2002 na kumaliza elimu yangu ya sekondari mwaka 2006 baadae niliendelea na kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari Bihawana mwaka 2007 na 2009 nikisomea mchapuo wa kilimo yaani CBA, (Chemistry, Biology and Agriculture ) Baadae ya kumaliza kidato cha sita nilifanikiwa kujiunga na Jeshi la Polisi Tanzania mwaka 2010 nikiingilia wilaya ya Chato Mkoani Kagera. Na mwaka 2010 kuajiriwa Jeshi la Polisi kuanza na Cheo kidogo Jeshini cha Police constable nikilitumikia Jeshi kwa uadilifu na nidhamu ya juu katika Wilaya ya Kongwa na Mkoa wa Dodoma.

ELIMU: Mnamo mwaka 2012 niliomba ruhusa ya kujiendeleza masomo ya jioni na kujiunga na Chuo Kikuu cha kilimo Morogoro ngazi ya Shahada ya Elimu ya kilimo kuanzia 2012 hadi 2015. Mwaka 2024 nilijiendeleza kielimu nakufanikiwa kupata Shahada ya Uzamili ya Mipango ya Miradi, Tathimini na Ufuatiliaji katika Chuo cha Maendeleo ya Mipango vijijini Dodoma.

MAJUKUMU: Kazi nilizowahi kufanya ni kama ifuatavyo nimefanikiwa kufanya kazi za Utawala katika ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma nikiwa kama Msaidizi wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma kuanzia mwaka 2017 hadi 2019. Nimefanikiwa kufanya kazi katika kitengo cha Intelijensia cha Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma nikiwa kama Incharge wa Operesheni zuia uhalifu toka mwaka 2019 hadi mwaka 2020.

CHEO: vyeo nilivyopanda ni kama ifuatavyo cheo cha Sgt wa Jeshi la Polisi mnamo mwaka 2021 na Cheo cha Mkaguzi wa Jeshi la Polisi mwaka 2025

MAFANIKIO: Nimefanikiwa kuandika tafiti tofauti (Research) katika dhana ya maendeleo kilimo Nchini fuatilia kwenye ukurasa wa LinkedIn. Kwa sasa najishughulisha uandaji tafiti mbalimbali kuhusu ukuaji wa uhalifu Nchini nimejikita katika uuelimishaji Jamii kuhusu dhana ya Polisi Jamii kwenye kuzuia na kupambana na uhalifu Nchini.