Mtumiaji:SAMWEL METANA

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chozi la marehemu

Nalikumbuka sana hadi leo,

Chozi lile la maendeleo,

Alilotoa bila kunywa kileo,

Alipoona limeibiwa koleo,

Siku kabla ya siku ya leo,

Chozi la marehemu kwetu.

Halikuwa la kawaida,

Japo alilitoa alipomuona dada,

Ilikuwa siku yake ya eda,

Kilio cha hali ya kawaida,

Aliona ndoa ya kaka na dada,

Ndipo lilipomtoka chozi.

Hata siku ile ya harusi,

Kaka wawili wakiwa maharusi,

Wakivaa shera na suti nyeusi,

Pasi kujali hali ya virusi,

Na kutoa kauli nyepesi,

Ni wapendanao hawa sasa,

Aliposimama kuliona,

Hakushudia hata aloyaona,

Kuku watano walonona,

Meno yakiwa yanasuguana,

Bila kupenda wala kujaliana,

Ndipo lilipomtoka pasi kujua.

Kwenye shida ya mpenzi wangu,

Siku zile akimuomba Mungu,

Ili amponye mpendwa mwanangu,

Aliyekuwa faraja maishani mwangu,

Japo aliondoka mikononi mwangu,

Chozi lako nalikumbuka sana.

Aliposikia migogoro

Kule morogoro,

Na ngorongoro,

Mwana kakosa karo,

Mkulima na mfungaji wa moro,

Walipopigana kisa sera mbovu.

Aliposikia mwanza hakuna samaki,

Musoma biashara kuu ni mapanki,

Wanae wala mifupa ya mabaki,

Hapo alipata tahamaki,

Leo minofu ulaya afrika mifupa yabaki,

Kilio chake kilivutia sana ndege.

Alinyamaza kimya siku ile,

Alipomuona mwenye kauli yule,

Akionesha shamba la wazee wale,

Bila kujali zao  kelele,

Masikitiko kwa watoto wale,

Walioachwa uchi chozi lako bado lipo.

                                          

                                           ( Metana S. D)