Mtumiaji:Mr phycian
Lugha fasaha Ni lugha inayozingatia kanuni za matamshi na maana sahihi lakini hutofautiana kutoka jamii moja na nyingine.Kwa mfanoMaandishi ya italiki i) katika jamii za Pwani,ukitamka neno “Bi mkubwa” lina maanisha “Mama mzazi” ii) katika jamii za Bara neno “Bi mkubwa” lina maanisha “Dada mkubwa wa Bibi ” iii) katika baadhi ya jamii “Bi mkubwa “ lina maanisha “Mke wa kwanza” mfano katika mikoa ya Singida,Rukwa,Songwe n.k Sifa za lugha fasaha Hutumika katika jamii husika Ina weza kuzingatia au isi zingatie lugha sanifu. Kwa hiyo: Matumizi ya lugha fasaha ni namna wazungumzaji wa lugha kwa kuzingatia kanunui za matamshi, muundo na mantiki katika kuzungumza. Matumizi ya lugha fasaha ni namna wazungumzaji wa lugha hutumia lugha kwa kuzingatia kanuni za matamshi, muundo na mantiki katika kuzungumza. . A) Onesha umuhimu wa kutumia lugha fasaha ya Kiswahili. Katika lugha fasaha, mawasiliano huwa na umuhimu ufuatao katika jamii; Hudumisha au huimarisha mahusiano baina ya wazungumzaji katika jamii. Hii husaidia kuimarisha mahusiano baina ya wazungumzaji ambao wapo katika jamii husika kwa kuzingatia mila na desturi zao.Kwa mfano wakati wa Hayat Rais Mkapa alipo kuwa ana fika katika jamii Fulani mfano kundi fulanii la vijana alikua anatumia salamu ambayo iliendana na kundi hilo kwa mafano alitumia neno “Mambo” hii ili saidia kudumisha uhusiano kati yake na wale vijana katika jamii ile ili aweze kufikisha ujumbe alio ukusudia kiurahisi zaidi. Huonesha utamaduni wa jamii husika. Hii hutambulisha utamaduni wa jamii Fulani.Kwa mafano mzungumzaji wa kutoka jamii “A” akienda jamii “B” akizungumza lugha ambayo anaitumia katika jamii yake anaweza kutambulika haraka kwamba anatoka katika jamii Fulani kulingana na aidha maneno ambayo ana yatumia kwa jamii hii nyingine.Mfano katika jamii za Pwani kutamka neno “Kunya”ni jambo ambalo lime zoeleka na lina onekana ni la kawaida, lakini kwa jamii za Bara uki tamka neno “kunya” lina weza kuwashangaza wasikilizaji wa jamii hii nyingine. Huonesha ustaarabu au kuelimika Kwa mtumiaji wa lugha fasaha. Hii ina mtambulisha mzungumzaji wa lugha fasaha katika jamii ambayo ana zungumza nayo.Kwa mfano matumizi ya tafsida katika baadhi ya maneno yanapo tumika katika jamii Fulani.Kwa mfano unapo taja neno sanifu hata kwenye kamusi maana yake imeelezwa kwa usahihi,ukalitumia katika jamii Fulani unaweza kuonekana huna madili au huna ustaarabu. Hudumisha taratibu za kisarufi za lugha. Lugha ya Kiswahili ina taratibu zake.Mfano mtu akisema “Juma hukuji shuleni leo” hajazingatia ufasaha wa lugha ingawa maana inaeleweka ila baadhi ya maneno ya tungo hiyo yana ukakasi kwa yeyote anejali ufasaha wa lugha.
B) Orodhesha changamoto ya matumizi ya lugha fasaha ya Kiswahili. • Kutamka vibaya maneno mfano mtu anasema “Mwalimu wa taaluma aliwakilisha taarifa ya wastani wa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba” Badala yakusema “Mwalimu wa taaluma aliwasilisha taarifa ya wastani wa ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba” • Kubadili maana ya neno au msamiati kwa mfano “Saida amenona” neno “nona” limetumika kimakosa kwa binaadamu baadala yake hutumika kwa mnyama anayefaa kuliwa kwa mfano mbuzi,ng’ombe,kondoo n.k • Kutokuwa na uelewa na utamaduni wa jamii husika. Hii hutokea pale ambapo mzungumzaji wa lugha Fulani anapo z ungumza lugha katika jamiii ambayo si yakwake inamuiya ugumu kuwasiliana na jamii ambayo ame ikuta. • Kuathiriwa Kwa lugha sanifu. Hapa lugha sanifu huwa haitumiwi mara kwa mara au haitumiki kabisa kwasababu inakuwa inaathiriwa na lugha fasaha.Kwa mafano mtu anaposema “Mashaka” ana maanisha wasiwasi au uwoga katika lugha fasaha lakini katika lugha sanifu “Mashaka” ina maana ya matatizo.
• Ina mtaka mzungumzaji kutumia lugha sanifu anapo kututana na jamii tofauti tofauti kwa wakati mmoja. • Kuzalishwa na kubadilika kwa misamiati mara kwa mara. Hii inapelekea jamii kuwa na misamiati mingi ambayo kwayo hutumika kwa muda mfupi kisha hupotea.Kwa mfano “Utajiju”, “Utajua hujui” “Fataki” , “Imeisha hiyo” n.k C) Fafanua mtindo wa kitaaluma Huu ni mtindo unaotumika katika mazungumzo na maandishi ya kitaaluma. Miktadha ya mazungumzo ya kitaaluma ni kama vile kwenye semina na makongamano ya kitaaluma, na katika utoaji wa mafunzo kwenye shule na vyuo. Maandiko ya kitaaluma ni kama vile vitabu vya masomo mbalimbali, kwa mfano Sayansi, Hisabati, Kiswahili na Historia. Mtindo huu, pia hutumika katika uandishi wa ripoti za kitaaluma, kwa mfano zinazohusu utafiti mbalimbali. Mtindo wa kitaaluma una sifa zifuatazo; i. Matumizi makubwa ya istilahi kulingana na eneo husika. Kwa mfano: Katika Kiswahili: Isimu, mofimu, nomino, kirai tenzi, kishazi, tungo, kiambishi. Sayansi: Kemia, kemikali, oksijeni, maada, kompaundi, elementi ii. Matumizi ya maneno ya mkopo ambayo ni ya kimataifa. Kwa mfano: haidroksaidi, mofolojia, ethinografia na leksikografia. iii. Matumizi makubwa ya wakati uliopo na wakati wa mazoea. Kwa mfano: Mwandishi wa riwaya anazungumzia kuhusu umaskini. Chakula kinapo fika tumboni huchanganywa na aside haidrokloriki. Dunia huzunguka jua kwa siku miatatu sitini na tano na robo. Oksijeni na haidrojeni zinapoungana huunda maji. iv. Matumizi ya nafsi ya tatu. Kwa mfano: Kikao kimeamua kuwa uteuzi wa wajumbe uahirishwe. Utafiti unaonyesha kwamba watu wengi wanapendelea chama hiki. v. Matumizi ya sentensi kamili (tungo) tofauti na ilivyo katika lugha ya mazungumzo ambayo hutumia kwa wingi sentensi za mkato. Pia matumizi ya sentensi zinazoficha mtenda. Kwa mfano: Imeamuliwa kuwa mjadala uendelee katika kikao kijacho. Inaaminika kuwa mwanadamu wa kwanza alitokana na sokwe. Inatarajiwa kuwa kila mwanachama atalipa mchango wake mapema. Inaeleweka kuwa mwaka uliofuata vita vilitokea. vi. Matumizi makubwa ya vitenzi. Kwa kawaida hapa hutumika vitenzi kuu kwa mfano: Jua huchomoza upande wa Mashariki na kuzama Magharibi. vii. Matumizi ya lugha yenye maana ya moja kwa moja, yaani isiyo na taswira, mafumbo, misemo, nahau, au methali. viii. Matumizi ya majedwali, vielelezo na michoro mbalimbali.
D) Fafanua mtindo wa kirasimu Mtindo wa kirasimu ni mtindo wa mawasiliano katika nyanja za utawala, uendeshaji wa uongozi pamoja na masuala ya kisheria ambayo yanafuata utaratibu fulani uliowekwa na sehemu husika. Mawasiliano haya yanaweza kutekelezwa kwa njia ya mazungumzo au maandishi.
Mtindo wa kirasimu ni ile namna ya mawasiliano yanavyotumika: • Kwa maofisini: Unapohitaji kuandika barua ya kiofisi unatumia manenoyafuatayo; kupitia kwa mwalimu mkuu, afisa elimu • Katika mahakama: Unahiatji kuchangia jambo lolote mahakamani ni sharti uanze na neno Mh. Hakimu • Katika dini kwa mfano wakristu wanapohitaji kufunga ndoa hufuata: Kuandikisha kanisani Kutangaza mara tatu kanisani Kusubiri pingamizi Kufunga ndoa Sifa za mtindo wa kirasimu: Matumizi ya mitindo iliyozoeleka kwa muda mrefu. Mtindo ambao umeanzishwa wakati huo huwa ni endelevu kwa kila atakayefuata katika matumizi. Mfano kwenye risala tunaandika: Ndugu Mgeni rasmi Mfano kwenye barua rasmi: Ndugu, Yah:, Wako mtiifu n.k Matumizi makubwa ya istilahi za kirasimu. Kwenye mtindo huu wa kirasimu huzingatia eneo husika unalohitaji kufikisha ujumbe. Mfano kwenye ofisi ya mkurugenzi utafuata utaratibu uliowekwa: Kufika ofisi ya masijala Kufika ofisi ya sekretari Matumizi ya sentensi ndefu. Kwenye mtindo wa kirasimu huwa na sentensi zenye maneno mengi. Mfano: Endapo upande mmoja kati ya pande hizi zilizoingia mkataba utapenda kujiondoa kwenye makubaliano haya, upande unaojiondoa utalipa upande unaobaki kiasi cha shilingi laki tano kama gharama za usumbufu utakaoletwa na kujitoa huko. Matumizi ya maneno yanayojaa vyeo. Katika mtindo huu unapotoa maelezo lazima uweke vyeo vya wahusika. Mfano: Mtendaji mkuu, Mkurugenzi mtendaji, Mwalimu wa taaluma Matumizi makubwa ya vitenzi jina. Katika mtindo huu wa kirasimu unapotoa maelezo yako mara nyingi hutumika vitenzi jina katika kufikisha taarifa uliyoikusudia. Kwa mfano wanachuo watakuwa na majukumu yafuatayo: Kulipa ada ya chuo kabla ya kusajiliwa Kufanya mitihani iliyoandaliwa na ofisi ya taaluma Matumizi makubwa ya maneno yanayodokeza maana. Katika mtindo huu huweza kutumika maneno yanayoelezea maana ya kitu au jambo kwa ufupi. Mfano: Kutokana na sheria ya chuo katika mtihani ili uweze kufanya mtihani wa mwisho lazima uwe na alama isiyopungua ishirini na tano katika somo husika na kwakuwa wewe una alama ishirini na mbili unatakiwa ufanye mtihani wa marudio alama zako kwenye somo husika.
E) Fafanua mtindo wa magazetini Magazeti ni chombo kinachotumia lugha ili kuwasiliana na jamii. Vilevile magazeti hutolewa kwa lengo la kibiashara. Magazeti kwa kawaida hutolewa kwa ajili ya siku moja tofauti na vitabu ambavyo huchapishwa mwaka hadi mwaka. Mtindo wa lugha ya magazetini huathiriwa kwa kiasi kikubwa na hali ya gazeti kushindwa kuuzwa siku inayofuata baada ya kuchapishwa. Hata hivyo, kwa ujumla wake tunaweza kusema kuwa magazeti hutumia mtindo wa lugha iliyopambwa na yenye mvuto mkubwa ili kunasa kwa urahisi hisia za walengwa. Zifuatazo ni sifa zinazobainisha mtindo wa magazetini Huchanganya mitindo mbalimbali, hii ni kwa sababu gazeti moja huwa na makala tofautitofauti. Kwa mfano, makala za kitaaaluma, michezo na matangazo ya biashara mtindo wa kitaaluma hutumiwa katika mazungumzo na maandishi ya kitaaluma.Miktadha ya mazungumzo ya kitaaluma ni kama vile kwenye semina na makongamano ya kitaaluma na katika utoaji wa mafunzo kwenye shule na vyuo. Matumizi ya tamathali za semi, ni matumizi ya maneno yenye maana kinyume na ile ya kawaida na yenye lengo la kutoa fundisho na kupamba sentensi kwa usanii.Pia ni matumizi ya maneno kwa namna fulani ili kuifanya lugha iwe ya kuvuitia na kuifanya kazi ya sanaa iwe ya kupendeza. Mifano ya tamathali za semi ni moja na “ Mjanja kama sungura”,”Mfupi kama nyundo”, “Mnene kama pipa”Kwa mfano, timu ya riadha waangukia pua, sumu ya kiongozi wa kijiji yaleta kizaazaa, mnyama awatafuna mwadui na serikali yamwaga mabilioni ya pesa. Matumizi ya simo (misimu), ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka na kutoweka kutegemea mazingira maalum. Misimu inayodumu huweza kuingia katika methali, nahau au misemo ya lugha ya jamii hiyo. Vyanzo vya misimu hutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayokumba jamii katika nyakati mbalimbali. Huzuka kutokana na hali ya utani miongoni mwa watu mbalimbali na mara nyingine misimu hubeba dhihaka, kejeli, mabezo, dharau au kusifu kusiko kwa kawaida. Kwa mfano, John anaswa laivu akipokea rushwa, kigogo wa kiwanda cha maji atimkia nchini Kenya, Yanga yamliza mtu na wananchi wapewa mwarobaini wa kuondokana na umaskini. Hutumia wakati uliopo kwa mambo ambayo tayari yameshapita.Mtindo huu hutumiwa kwa lengo la kuwavutia wasomaji.Habari itakapoandikwa kwa kutumia wakati uliopita wasomaji hupunguza ari ya kutaka kujua maudhui kwani mambo mengine huwa wameshapata taarifa au ujumbe huo.Kwa mfano, Afisa elimu akemea walimu wazembe,ajali yaua saba, Manara atikisa taifa. Matumizi ya vitenzi jina, mara nyingi Virai nomino hutumika kuelezea tendo litakalo fanyika wakati ujao. Uandishi wa vichwa vya habari magazetini Kwa kutumia Virai nomino ili kuonyesha wakati ujao vilevile hutumika sana. Mifano: Rais kwenda Nairobi leo yaani ataondoka leo mchana.Kwa mfano, sensa kufanyika mwezi wa nane, serikali kuagiza mtambo wa kufua umeme, wananchi waishio mabondeni kuhamishwa na kigogo kuburuzwa mahakamani. Matumiza ya visawe mbalimbali vya maneno. Visawe ni uhusiano wa maneno yenye maana zinazo karibiana lakini maumbo na matamshi ni tofauti. Kwa mfano, jambazi akamatwa/ latiwa nguvuni/ lanaswa au laangukia mikononi mwa sheria. Mpira wa miguu/kabumbu/soka au gozi. Timu yafungwa/ yanyukwa/ yabugizwa mabao/ yashindiliwa magoli/ yabamizwa / yatwangwa/ yakubali kipigo.
F) Fafanua mtindo wa mazungumzo yasiyo rasmi.
Mazungumzo yasiyo rasmi
Mazungumzo yasiyo rasmi, Ni yale maongezi ya kawaida ya kila siku. Mfano:
• Nyumbani (yaani mazungumzo kati ya baba na mama, watoto, watumishi wa nyumbani n.k)
• Kijiweni.
• Vimbwetani.
• Kumbi za starehe.
Sifa za mtindo wa mazungumzo yasiyo rasmi
Sifa zisizo za kiisimu
Kutokuwepo kwa mazingira rasmi ya mawasiliano,
Yaani watu wanaowasiliana lazima wajisikie huru na hawabanwi na hali yoyote inayowalazimisha kutumia dhana fulani tu za kiisimu, Mfano barua kati ya marafiki wawili kuhusu maisha yao ya kawaida ya kila siku.
Mada ni nyingi na nyingine huzuka papo kwa papo.Hapa wazungumzaji hawazingatii mada moja wakati wa mazungumzo yao, mada inayo zingumzwa awali huachwa na kuingizwa mada mpya katika mazungumzo.
Kuchanganywa kwa lugha.Hapa wazungumzaji hawatumii lugha moja katika mazungumzo yao.Mzungumzaji anaweza hata kutumia lugha ya kikabila wakati wa mazungumzo au hata kutumia lugha ya kiingereza.
Tungo zake kukatishwa wakati wa mazungumzo.Kwa mfano unaweza ukawa upo katika mazungumzo, kabla hujamaliza kuzungumza jambo la mwanzo unakatishwa na kuambiwa jambo jingine.
Hakuna istilahi nyingi kwa kuwa huzungumzia mambo ya mtaani zaidi.
Uwezekano wa kubadilisha mada bila madhara.
G) Mambo ya kuzingatia wakati unapoteua mtindo wa kutumia katika miktadha tofauti ni; 1) Muktadha Msemaji wa lugha yoyote ile anakuwa katika mazingira yanayomtawala kimaisha. Muktadha huo ndio unao mwamlia kuhusu vitendo na hata mazungumzo yake kutokana na muktadha. Tunaweza kupata lugha ya hotelini, lugha ya shuleni, lugha ya ofisini, lugha ya kanisani, lugha ya mitaani n.k Mfano lugha ya mtaani imejaa maneno ya mitaani ambayo yanaeleweka kwa wazungumzaji wenyewe. Mfano; Ee bwana we! Maana hiyo benzi ilikuja kitutu – wangu wangu! Bila kutazama mbele Kinakuja nini, basi akamwingia babu wa watu – akamrusha kama mpira, na alipofika chini, kwisha habari yake! Kichwa Kama chapatti, Simba wa mji watatumaliza!
2) Uhusiano baina ya wahusika Uhusiano baina ya wahusika pia ni jambo la kuzingatia unapoteua mtindo wa kutumia katika mazungumzo. Hapa mazungumzo au lugha utakayotumia itategemea unaongea na nani. Kutokana na uhusiano wa wahusika tunapata; Lugha ya baba na mtoto, Lugha ya watu wenye rika moja, Lugha ya mtu na mpenzi wake. Lugha ya mwalimu na mwanafunzi wake, Lugha ya meneja na wafanyakazi wa chini yake. Mfano lugha ya watu wa rika moja wanazungumza lugha ambayo wenyewe wanaelewa na sio rahisi mtu wa rika nyingine kuelewa lugha hiyo Mfano
”Big tunasikia unamisi skuli siku hizi ni kwa nini”
“Ah, si Yule ticha sululu………….eti kanipakazinimechapa daftari ya shule” “Maticha wote wakapanga wanishike ili wanibiti, lakini niliwatoka mfano roketi” “Chekini washikaji, dingi angenou si ingekuwa hatari, khatari!” “Ngoja niwape siri, ninamisheni baba K kuwabamiza wale maticha, lakini msitoe siri hii sawa?” “No sweat. Mtu usomapo maelelezo hayo, mara moja unaona jinsi vijana hawa wa rika moja waishio mijini wanavyozungumza Kiswahili. Si rahisi kwa mzungumzaji wa Kiswahili sanifu kuelewa kirahisi lugha hiyo
3) Mada ya mazungumzo Kimsingi mada ya mazungungumzo hutawala usemaji na jinsi ya uzungumzaji kwa ujumla kutokana na mada ya mazungumzo tunapata lugha ya; Kibiashara, Kitaaluma, Mahubiri, Kisiasa, Kisheria n.k Mfano: Lugha ya kisheria – Mazungumzo kati ya wakili na mwendesha mashitaka JUMA: Nakuuliza jaribio la kutaka kupindua serikali litakuwa la na namna gani katika sheria za Tanzania?
ALLY: Ni kosa la uhaini.
4) Madhumuni ya mazungumzo Hapa mzungumzaji hutoa ufafanuzi wa yale anayotaka kusema. Hivyo ufafanuzi huo utategemea madhumuni ya mazungumzo hayo. Kwa mfano mazungumzo hayo yana lengo la kutoa hamasa ambayo yanaweza kuoneshwa kwa kupitia sura na mwili wako ili kufikisha ujumbe uliokusudia: Mfano: Unahitaji kuwasilisha jambo lolote katika hadhira
5) Jinsi mawasiliano yanavyo fanyika. Namna ya mawasiliano yanavyofanyw kwa maandishi au mazungumzo utaathiri jinsi au mtindo wa uzungumzaji. 6) Muda wa mazungumzo Mazungumzo yanayotolewa yaendane na muda uliokusudiwa kwa lengo la kufikisha taarifa au ujumbe ambao umekusudiwa kufikishwa kwa jamii. Kwa mfano katika midahalo mbalimbali hupangiwa muda maalum wakati wa uwasilishaji wa mada, hivyo unapaswa kuzungumza mambo yanayohusu mada hiyo na sio vitu vya nje ya mada husika. 7) Wakati wa mazungumzo yanapofanyika Mazungumzo yanapofanyika lazima yaoneshe wakati wa mazungumzo yanapofanyika kwa lengo la kuonesha wakati sahihi wa mazungumzo au matukio. Kwa mfano: Unapoeleza tukio lililotokea wakati uliopita, leo, asubuhi, ujao 8) Uwezo wa mtu au mzungumzaji Unapofanya mazungumzo unatakiwa kuzingatia uwezo wa mzungumzaji katika kuifahamu lugha. Kwa mfano kuwa na uwanja mpana katika misamiati na matumizi ya lugha ipasavyo. 9) Hali ya mazungumzo Mazungumzo yanapofanyika huzingatia utayari wa wasikilizaji.Kwa mfano mazungumzo yatapofanyika msibani yatazingatia hali ya wafiwa, unapokuwa kwenye mahafali utapaswa kufanya mazungumzo yanayoendana shughuliMaandishi ya kooze