Mtumiaji:Madaraka Masasi/Kilimani Sesame
Kilimani Sesame ni toleo la Kitanzania la kipindi cha Sesame Street. Kipindi hiki hurushwa hewani kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Televisheni Zanzibar (TVZ). Uzalishaji wa kipindi hiki ulizinduliwa mwezi Aprili mwaka 2008. Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) lilifadhili uzalishaji huu.
Uzalishaji
[hariri | hariri chanzo]Kipindi hiki kinaonesha vipengele vilivyorekebishwa kutoka katika uzalishaji wa pamoja wa Afrika Kusini, Takalani Sesame, vilivyotafsiriwa kwa Kiswahili. Sehemu za uhalisia (live action) hutayarishwa na wazalishaji wa ndani, kwa msaada wa Maweni Farm, kampuni ya utayarishaji wa filamu na ushauri.
Ujumbe
[hariri | hariri chanzo]Kuzuia malaria na elimu ya VVU/UKIMWI ndizo sehemu kuu mbili za kielimu za programu hii. Mada nyingine ni pamoja na kujua kusoma na kuandika na hisabati.
Programu hii ni sehemu ya Mpango wa Kimataifa wa Kupambana na Malaria (Global Malaria Action Plan - GMAP) chini ya Ushirikiano wa Roll Back Malaria. Mashirika mengine ambayo kipindi hiki kimeshirikiana nayo ni Taasisi ya Jane Goodall Tanzania/Roots and Shoots Program, Pact Tanzania, na Children and Youth Development Initiative.