Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Jamesmwakila/ukurasa wa majaribio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
James Buchanan
Ryan Lane na Katie Leclerc katika hafla ya msaada wa Mbwa kwa Viziwi mnamo Aprili 2013.
Ryan Lane na Katie Leclerc katika hafla ya msaada wa Mbwa kwa Viziwi mnamo Aprili 2013.
Jina la kuzaliwa Ryan Thomas Lane
Alizaliwa 1791
Alikufa 1868
Nchi Marekani
Kazi yake Rais
Wazazi James Buchanan Sr. na Elizabeth Speer
Tovuti rasmi LancasterHistory – Makumbusho ya Nyumbani kwa Rais James Buchanan (Wheatland)

James Buchanan Jr.[1] (Aprili 23, 1791  Juni 1, 1868) alikuwa Rais wa 15 wa Marekani, akihudumu kuanzia mwaka 1857 hadi 1861. Pia aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuanzia 1845 hadi 1849 na aliwakilisha Pennsylvania katika mabaraza yote mawili ya Bunge la Marekani[2]. Buchanan alikuwa mtetezi wa haki za majimbo, hasa kuhusu suala la utumwa, na alipunguza jukumu la serikali ya shirikisho kabla ya kuzuka kwa Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani[3].

Buchanan alikuwa wakili huko Pennsylvania na alishinda uchaguzi wake wa kwanza kuingia katika Baraza la Wawakilishi la jimbo kupitia Chama cha Federalist. Alichaguliwa katika Baraza la Wawakilishi la Marekani mwaka 1820 na alihudumu kwa mihula mitano, akijiunga na Chama cha Democrat cha Andrew Jackson. Mnamo 1832, aliteuliwa kuwa balozi wa Marekani nchini Urusi.

Mnamo 1834 alichaguliwa kuwa seneta wa Marekani kutoka Pennsylvania, nafasi aliyoshikilia kwa miaka 11.Mnamo 1845, Rais James K. Polk alimteua kuwa waziri wa mambo ya nje, na mwaka 1853 alitumwa na Rais Franklin Pierce kuwa balozi wa Marekani nchini Uingereza.

  1. Olausson, Lena; Sangster, Catherine (2006). Oxford BBC Guide to Pronunciation. Oxford University Press. uk. 56. ISBN 0-19-280710-2.
  2. https://books.google.co.tz/books?id=yX7Ih0EQUaQC&pg=PA214&redir_esc=y#v=onepage&q&f=false
  3. https://books.google.co.tz/books?id=cdgmDAAAQBAJ&pg=PA23&redir_esc=y#v=onepage&q&f=false