Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Iran Cultural Centre

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran hapa nchini  kinapenda kuwataarifu wapendwa wasomaji wa mitandao ya kijamii kuwa kimefungua Ukurusa wake rasmi wa WIKIPEDIA ili kuwapa taarifa wasomaji jinsi gani kinavyoendesha shughuli zake mbalimbali za Kiutamaduni hapa nchini.

Historia fupi ya uanzishwaji wake.

Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam ya  Iran kimeanzishwa mnamo mwaka 1986 ikiwa ofisi yake ya kwanza ikipatikana katika Barabara ya Mazengo Upanga jijini Dar es Salaam.

Malengo ya uanzishwaji wake

Kabla ya kuanzishwa kwa Kituo hiki shughuli zote za Kiutamaduni na dhifa mbali mbali za kitaifa za Jamhuri ya Kiislam ya Iran ziliratibiwa na kusimamiwa  na Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislam hapa nchini, ndipo pakatokea haja ya ulazima kutenganisha kati ya shughuli za kiutamaduni na zile zenye mafungamano ya kitaifa haya mawili. Hapo pakawa ni msingi wa kuanzishwa kwa Taasisi hii muhimu na adhimu ili kuratibu shughuli zote za Kiutamaduni kati ya mataifa haya mawili Iran na Tanzania.

Ikiwa na Jukumu kuu la kujenga na kuimarisha uhusiano wa historia na utamaduni uliokuwepo baina ya wananchi wa mataifa haya mawili pia kukuza na kuenzi fikra za waasisi wa mataifa haya mawili ambao ni  Ayatollah Imam Khomeini (R.A) muasisi wa Mapinduzi ya Jamhuri ya Kiislam ya Iran  na Marehemu Mwalim Julius K. Nyerere na pia kushirikiana na Serikali, Taasisi za Umma na Binafsi pamoja na wadau mbalimbali wa Utamaduni na sanaa katika kujenga uhusiano mwema kati ya Wananchi wa Mataifa haya mawili kupitia Sanaa na Utamaduni.

Mahali Kilipo Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Upanga, Barabara ya Ali Hassani Mwinyi karibu na kituo cha Mabasi (Daladala) cha Palm Beach

Mawasiliano.

Sanduku la Posta 7898, Dar es Salaam - Tanzania

Namba za Simu: +2552136677

Barua pepe: daressalaam@icro.ir

Tovuti: en.daressalaam.icro.ir