Mtumiaji:ELIKANA EMANUELI SIMA LIMU
Elkana Emmanuel Sima (alizaliwa tarehe 19 Juni 2002) ni mwalimu na mwanaharakati wa maendeleo ya jamii kutoka Tanzania. Kwa sasa anahudumu kama mwalimu wa masomo ya Jiografia katika shule ya sekondari ya Iguguno, Wilaya ya Mkalama, mkoa wa Singida. Amekuwa mstari wa mbele kusaidia wanafunzi kitaaluma na kujihusisha na shughuli za kijamii katika kata ya Iguguno.
Historia ya maisha na elimu: Elkana alizaliwa katika hospitali ya St. Carolus, Singida akiwa ni mtoto wa kwanza kuzaliwa kwenye familia yao. Wazazi wake ni Emanuely Sima Limu na Elifrida Jackson Muna. Alikulia na kuishi kata ya Iguguno. Alisoma shule ya msingi Sophia iliyopo mkoani Singida, kisha kujiunga na Shule ya Sekondari Iguguno iliyopo mkoani Singida kwa elimu ya sekondari na baadae kujiunga na Shule ya Sekondari iliyopo Alfa kwa ajili ya elimu ya kidato Cha tano na sita. Mwaka 2021 alihitimu elimu ya kidato Cha sita katika shule ya Sekondari Alfa iliyopo mkoani Morogoro na kujiunga na JKT mujibu wa sheria katika kikosi cha Makutupora 834KJ, Dodoma, na mwaka huo huo 2021 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kusoma Shahada ya kwanza katika elimu na kuhitimu mwaka 2024.
Kazi: Baada ya kuhitimu alianza kufundisha shule ya sekondari ya Iguguno mnamo tarehe 29 July 2024 akifundisha somo la Jiografia. Mnamo mwaka 2025 alipatiwa zawadi na mkuu wa shule kwa kufaulisha wanafunzi wa kidato cha pili katika mtihani wa kitaifa wa FTNA mwaka 2024.
Siasa: Mwaka 2025, aligombea nafasi ya Udiwani katika kata ya Iguguno kwa lengo la kuendeleza miradi ya maendeleo ikiwemo elimu, afya, kilimo na mikopo kwa vijana.
Mitandao ya kijamii: Anapatikana katika majukwaa mbalimbali ya kijamii kama Wikipedia, Facebook, Instagram, Threads, TikTok, LinkedIn, "School and College Listings" na Sciprofile.