Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Ccmpple

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
William Andrews
Amezaliwa 10 Oktoba 1977
Salisbury rhodesia
Kazi yake Mchekeshaji

William Andrews (alizaliwa tarehe 10 Oktoba 1977 huko Salisbury, sasa Harare, katika koloni la zamani la Waingereza lililojulikana kama Rhodesia, sasa Zimbabwe) ni mwigizaji na mchekeshaji wa Kizungu kutoka Uingereza.[1][2]

Andrews alihudhuria Chuo cha Sanaa cha Edinburgh, ambako alipata Shahada ya Sanaa katika Upigaji Picha.

Alishinda Tuzo[3] za Tap Water kwa ucheshi wa kuigiza wahusika kwenye Tamasha la Edinburgh Fringe la mwaka 2003, akicheza kama Tony Carter, Mwingereza asiye na bahati kutoka Geordie. Mwaka 2007, alishinda tuzo ya BAFTA[4] ya Uskochi kwa nafasi yake katika kipindi cha televisheni cha Blowout.

Anaigiza katika tamthilia ya vichekesho ya watoto ya BBC inayoitwa Sorry, I've Got No Head, akiwa na David Armand, James Bachman, Marcus Brigstocke, Anna Crilly, Justin Edwards, Mel Giedroyc, Marek Larwood na Nick Mohammed. Pia aliigiza katika Pixelface. William Andrews pia ni mjumbe wa bodi ya The Alternative Comedy Memorial Society.

Mwaka 2022, alionekana kama Josiah katika sehemu moja ya mfululizo wa 4 wa kipindi Ghosts.[5]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtumiaji:Ccmpple kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. https://en.m.wikipedia.org/wiki/Chortle
  2. https://en.m.wikipedia.org/wiki/Chortle
  3. http://www.tapwaterawards.org/winners.html
  4. https://en.m.wikipedia.org/wiki/BAFTA_Scotland
  5. https://www.bbc.co.uk/iplayer/episode/m001cld0/ghosts-series-4-2-speak-as-ye-choose