Mtumiaji:Capricorn94

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utofauti wa vizazi[hariri | hariri chanzo]

Utofauti wa vizazi ni utofauti wa kimtizamo kati ya kizazi kimoja na kizazi kingine kiimani, kisiasa au kimatabaka. Kwa matumizi ya leo, utofauti wa vizazi unaonekana ni utofauti kati ya vijana na wazazi au wazee.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kati ya Sosholojia wa mwanzo kama Karl Mannheim aliona tofauti kwenye vizazi mbali mbali kwa namna vijana wanavyopitia ujana kwenye kwenye utuuzima na akajifunza njia ambazo vizazi wanajitenga na vizazi vingine majumbani, makanisani, makundi ya watu wazima na makundi ya vijana.

Nadharia ya kisosholojia ya utofauti wa vizazi ilikuja kwa mara ya kwanza mwaka 1960 wakati vizazi vidogo walikuwa wakienda tofauti na vitu vingi ambayo wazazi wao walikuwa wakiamini kwa nyanja mbali mbali kama kimuziki, kisiasa na kitamaduni.

Kutenganisha utofauti wa vizazi[hariri | hariri chanzo]

Kuna njia mbali mbali za kutofautisha vizazi. Kwa mfano majina wanayopewa makundi mbali mbali ya vizazi kama (vizazi kimya, vizazi X, vizazi milenia na vizazi alfa) na kila vizazi huwa na uvumi wao pamoja na athari kati jamii zao.


Matumizi ya lugha

Inaweza kutofautishwa kwa matumizi yao ya lugha. Utofauti wa vizazi umeleta utofauti kwenye lugha unaosababisha ugumu kuwasiliana. Tatizo hili limeonekana kwenye jamii na kusababisha mkingamo kwenye mawasiliano ya siku na siku, majumbani, mashuleni na makazini

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.dictionary.com/browse/generation-gap
  2. https://books.google.com/books?id=FYElqUmQttgC