Nenda kwa yaliyomo

Mtumiaji:Brebre93/Fatma Juma Haji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fatma Juma Hajializaliwa (tarehe5 mwezi wa 6 mwaka 1965) kisiwani Pemba. Fatma kwa sasa ni mkufunzi wa umeme wa jua pamoja na meneja kituo cha umeme wa jua kiitwacho Barefoot kilichopo Kinyasini Kibokwa, mkoa wa Unguja [1]

Elimu Fatma Juma Haji hakupata bahati ya kusoma mpaka mwaka 2011 alivyochaguliwa kutoka kijijini cha Kandwi, Unguja kwenda nchini India kujiunga na masomo ya umeme wa jua.

Baada ya masomo Baada ya masomo ya umeme wa jua yaliyodumu kwa miezi sita nchini India, Fatma alirudi na kuajiriwa na chuo cha Barefoot kama mkufunzi wa umeme wa jua kazi kubwa ikiwa ni kufunga vifaa vya umeme wa jua vijiji tofauti kisiwani Pemba na Unguja. Mpaka sasa Fatma Juma Haji ameweka vifaa vya umeme wa jua kwenye nyumba zaidi ya mia mbili visiwani humo. Tofauti na visiwani, Fatma ameenda pia nchi ya Sudan kusini kusaidia wakufunzi wa umeme wa jua kufunga umeme katika vijiji mbalimbali nchini humo.

Hivi Sasa Fatma Juma Haji ameendelea kuweka nuru katika vijiji mbalimbali katika visiwa vya Unguja na Pemba. Pia Fatma amepata mialiko kutoka sehemu tofauti, alialikwa nchi ya Urusi kwa week mbili (2) kufundisha wamama tofauti kuhus umeme wa jua. Mwaka 2019 Fatma Juma Haji alipata mwaliko wa kuhudhuria nchi ya Ufaransa kuelezea kuhusu shughuli mbalimbali anazozifanya kuendeleza vijiji kwa kuwapa nuru ya umeme wa jua.