Mtumiaji:AndyTanzania
HOMBOLO VILLAGE IN DODOMA
Hombolo ni kijiji kinachopatikana huko mkoani Dodoma wilaya ya Dodoma mjini.Kijij hiki kina wakazi wenye asili tofauti tofauti ilakwaasilimia kubwa kimekaliwa na wagogo ambao kwa asili ndio wazawa wa eneo hili.Wakazi wa kijiji hiki wanategemea sana shughuri ya kilimo cha mahindi,alizeti ,zabibu pamoja na shughuri ya kilimo.Shughuri ya kilimo imegawanyika katika sehemu mbili ambapo kuna kilimo cha umwagiliaji pamoja na kilimo cha kutegemea mvua za msimu,kilimo cha umwagiliaji kinahisisha kilimo cha mboga mboga na matunda paoja na kilimo cha zabibu ambapo kwa kiasi kikubwa wakazi wa kijiji hiki. wamekuwa wakijinasua kutoka katika lindi la umasikini.Serikali kwa kutambua mchango wa kilimo cha zabibu kutoka katika kijiji cha Hombolo wakaamua kujenga kiwando cha mvinyo ambacho kimekuwa mchango mkubwa kwa wanachi wanaokizunguka kiwanda hiko kwani vijana wengi wamepata ajira kutoka katika kiwanda hicho cha kutengeneza mvinyo.Kijij cha Hombolo pia kimepata bahati ya kuwa na bwawa ambalo lilichimbwa miaka ya 1950 bwawa hili limekuwa mkombozi kwa wakulima na wafugaji.Kwa kutambua hali nzuri ya mazingira serikali ya jamhuri ya muungano waliamua kujenga chuo kikubwa cha serikali za mitaa kinachoitwa Local government traing institute.Wazee maarufu wa kijiji cha Hombolo ni mzee Andrea Luhamo,mzee Lechipya,mzee Nonya,Mzengo na wengineo wengi.