Ninaamini katika nguvu ya maarifa, na ndoto yangu ni kuona maarifa ya mtandaoni yanapatikana kwa lugha ya Kiswahili kwa kila mtu bila vizuizi vya lugha wala teknolojia. Kupitia uhariri wangu, nalenga kusaidia jamii kupata taarifa sahihi, zinazowezesha na kuelimisha.
Mimi pia ni mwanzilishi wa Cyber Swahili[2], jukwaa linalotoa elimu ya usalama wa kidijitali, matumizi bora ya teknolojia, na uelewa wa mitandao kwa vijana, wazazi, na walimu. Kupitia kazi hii, ninahamasisha matumizi salama ya intaneti na maadili ya kidijitali kwa jamii.
Ninajihusisha pia na malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) [3]hasa Lengo la 4: Elimu Bora, nikiamini kuwa elimu salama, jumuishi, na ya kidijitali ni haki ya msingi kwa kila mtu.
↑ "Mwanzo", Wikipedia, the free encyclopedia, 2023-04-24, iliwekwa mnamo 2025-07-18,
Mchangiaji wa kujitolea wa Wikipedia ya Kiswahili na miradi mingine ya Wikimedia, akichangia maendeleo ya maarifa kwa lugha ya Kiswahili.
↑ "CyberSwahili". CyberSwahili (kwa Kiingereza). 2025-07-16. Iliwekwa mnamo 2025-07-18.
Cyber Swahili ni mradi unaolenga kuelimisha jamii kuhusu usalama wa mtandao na matumizi bora ya teknolojia.