Tondi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mtonzi)
Tondi
Tondi milia (Plotosus lineatus)
Tondi milia (Plotosus lineatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Siluriformes (Samaki kama kambale)
Familia: Plotosidae
Bleeker, 1858
Ngazi za chini

Jenasi 10, spishi 41:

Tondi, mitonzi au mitozi ni samaki wa baharini na maji baridi wa familia Plotosidae katika oda Siluriformes wanaofanana na mikunga lakini kuwa na sharubu kama kambale. Huitwa ngogo pia lakini jina hili tafadhali litumike kwa jenasi Synodontis.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Tondi wana mwili kama mkunga. Mkia wao una ncha kali au butu. Takriban spishi zote zina jozi nne za sharubu. Pezi lenye shahamu halipo. Pezi la mkia limeundwa kwa kujiunga kwa pezimgongo la pili, pezimkia na pezimkundu katika pezi moja bila pengo. Baadhi ya samaki hawa huweza kusababisha vidonda vinavyoumia; kudungwa na tondi milia kunaweza kupelekea kifo. Hujilisha kwa sakafu ya maji na kutumia sharubu pande zote za kinywa chao ili kugundua chakula.

Msambao[hariri | hariri chanzo]

Tondi wanaoishi baharini wanatokea Bahari ya Hindi kutoka pwani ya Afrika ya Mashariki mpaka Australia, Japani na Fiji katika Bahari ya Pasifiki. Takriban nusu ya spishi zote hutokea maji baridi katika Australia na Nyugini.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tondi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.