Mto Tajo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mto Tajo, Tejo
Chanzo Fuente Garcia, Teruel, Hispania
Mdomo mjini Lisbon katika Atlantiki
Nchi Hispania, Ureno
Urefu km 1,007
Kimo cha chanzo m 1,627
Mkondo m 3 500
Eneo la beseni km2 80,100
Tajokaribu na mpaka wa Hispania - Uremo

Mto Tajo (pia: Tejo; kwa Kihispania: Tajo; kwa Kireno: Tejo; kwa Kiingereza: Tagus) ni mto mrefu zaidi katika rasi ya Iberia yaani kwenye nchi za Hispania na Ureno. Urefu wake ni km 1,007 kwa jumla, ikiwa km 716 ziko nchini Hispania na km 275 huko Ureno. Kwa km 47 mto huu ni mpaka kati ya Ureno na Hispania. Tejo inaishia katika ya Bahari Atlantiki karibu na mji mkuu wa Ureno, Lisbon.

Beseni lake ni km2 80,100. Tajo-Tejo hutumiwa sana kwa shughuli za umwagiliaji katika sehemu inapopita kozi yake yote. Mabwawa kadhaa yanakusanya maji ya kunywa kwa maeneo mengi ya Hispania, pamoja na Madrid, na ya Ureno. Kuna vituo kadhaa vya umeme vinavyotengeneza umeme. Kwenye mdomo wake baharini mto unapanuka sana na ndipo bandari ya Lisbon inapopatikana.

Chanzo cha Tajo kipo katika milima ya Mkoa wa Teruel nchini Hispania. Miji mikubwa zaidi ambako hupitia ni Aranjuez, Toledo, Talavera de la Reina na Alcántara huko Uhispania, halafu Abrantes, Santarém, Almada na Lisbon huko Ureno.

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Tajo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.