Nenda kwa yaliyomo

Mto Sebou

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani inayoonyesha eneo na mwendo wa Mto Sebou kaskazini mwa Moroko

Mto Sebou (pia Mto Guigou), ni mto uliopo kaskazini mwa nchi ya Moroko. Katika eneo la chanzo chake kwenye milima ya Atlas ya Kati [1]. Mto huu una urefu wa kilomita 496 na una wastani wa mtiririko wa maji wa mita za ujazo 137 kwa sekunde, jambo linalofanya mto huu kuwa mto mkubwa zaidi upande wa kaskazini mwa Afrika katika nyaja ya ujazo wa maji.

Mto Sebou unapita karibu na mji wa Fes, ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Moroko, na unamwaga maji yake katika Bahari ya Atlantiki kwenye eneo la Mehdya. Mto huu unafaa kwa usafiri wa vyombo vya majini kwa umbali wa kilomita 16 tu hadi kufikia mji wa Kenitra, ambao una bandari pekee ya mtoni nchini humo. Matawi muhimu zaidi yanayomwaga maji kwenye mto huu ni pamoja na Mto Ouergha, Mto Baht, na Mto Inaouen. Pia, mto huu unasaidia sana shughuli za umwagiliaji katika ukanda wenye ardhi yenye rutuba zaidi nchini Moroko unaojulikana kama Gharb.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa zamani, Mto Sebou ulijulikana kwa jina la *Sububus*. Mwandishi wa kale Pliny Mzee alieleza kuwa mto huo ulikuwa mkuu na ukafaa kwa usafiri wa meli ("magnificus et navigabilis"), ukitiririka karibu na miji ya kale ya Banasa na Thamusida.[2][3]

Kuna kumbukumbu chache sana za kihistoria zinazoonyesha matumizi ya mto huu kwa usafiri wa majini baada ya upanuzi wa Uislamu katika ukanda huo; hata hivyo, mdomo wa mto huu ulikuwa bandari muhimu na eneo la kuundia meli wakati wa utawala wa nasaba ya Almohad. Katika miaka ya 1669–1670, Sultani Moulay Rashid wa nasaba ya Alaouite alijenga daraja kubwa juu ya mto huu karibu na mji wa Fes ambalo bado limehifadhiwa hadi leo.[4][5][6][7]

Kabla ya kipindi cha ukoloni, mto huu ulijulikana sana kwa kuwa na samaki aina ya "Twait shad" ambao walipendwa sana na wakazi wa Fes, lakini walitoweka kabisa kutokana na uchafuzi wa mazingira mtoni. Katika miaka ya kwanza ya utawala wa ulinzi wa Kifaransa, msafara mmoja ulifanikiwa kupita kwenye mto huu kwa kutumia boti ndogo ya mvuke kutoka Sidi Ali Ben Sliman hadi jiji la Fes.

Uhifadhi na changamoto za mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Mfumo wa ikolojia wa mto huu unakabiliwa na changamoto kubwa za kiutunzaji ambazo zinaathiri rasilimali za maji safi nchini Moroko. Kiasi kikubwa cha uchafuzi huingia kwenye Mto Sebou, hususan viuatilifu na mbolea za kemikali zinazosombwa na maji kutoka kwenye mashamba makubwa ya kilimo, pamoja na majitaka ambayo hayajasafishwa yanayotiririshwa kutoka kwenye miji iliyo kando ya mto huo.[8] Juhudi za kiuhifadhi zimekuwa zikihitajika ili kulinda bonde hili la mto kwa ajili ya kilimo endelevu na afya ya jamii.

  1. "Sebou River". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 2 Desemba 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Pliny the Elder. Natural History, book V (kwa Kilatini). Iliwekwa mnamo 6 Januari 2019.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Natural History, book V, translated (kwa Kiingereza).
  4. Gaudio, Attilio (1982). Fès: Joyau de la civilisation islamique. Paris: Les Presse de l'UNESCO: Nouvelles Éditions Latines. ISBN 2723301591.
  5. "Pont Oued Sebou". Inventaire et Documentation du Patrimoine Culturel du Maroc (kwa Kifaransa). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-07-28. Iliwekwa mnamo 2020-07-28.
  6. Le Maroc de 1631 à 1812: extrait de l'ouvrage intitulé "Ettordjemân elmoʿarib ʿan douel elmachriq ou ʿlMaghrib de Aboulqâsem Ben Ahmed Ezziani. Ilitafsiriwa na Houdas, Octave Victor. École des langues orientales vivantes. 1886. uk. 21.
  7. Marçais, Georges (1954). L'architecture musulmane d'Occident. Paris: Arts et métiers graphiques.
  8. Thieme, Michele & Abell, Robin & Stiassny, Melanie & Skelton, Paul. (2005). Freshwater Ecoregions of Africa and Madagascar: A Conservation Assessment. Bibliovault OAI Repository, the University of Chicago Press. 1–431.
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Sebou kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.