Mtakatifu Mauro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
"Mt. Benedikto akimuagiza Mt. Mauro kwenda kumuokoa Mt. Plasido", mchoro wa Filippo Lippi, O.Carm. (1445 hivi).

Mtakatifu Mauro, O.S.B. (512-584) alikuwa mfuasi wa kwanza wa Benedikto wa Nursia, kama inavyoelezwa na Gregori Mkuu katika masimulizi manne juu yake ambayo yalitumika sana baadaye katika malezi ya Wabenedikto.

Humo tunasikia kwamba wazazi wake walikuwa wa koo bora za Roma wakamtoa bado mtoto monasterini ili afuate maisha ya kitawa.

Baadaye alijitokeza kwa utiifu wake kwa abati wake na hata kwa miujiza mbalimbali.

Habari nyingi zaidi zilitungwa katika karne ya 9 lakini si za kuaminika.

Anaheshimiwa kama mtakatifu tarehe 15 Januari, au, pamoja na mwenzake Plasido, tarehe 5 Oktoba.[1]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum (Libreria Editrice Vaticana 2001 ISBN 88-209-7210-7)

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Gardner, Edmund G. (editor) (1911. Reprinted 2010). The Dialogues of Saint Gregory the Great. Merchantville, NJ: Evolution Publishing. 
  • Rosa Giorgi; Stefano Zuffi (ed.), Saints in Art (Los Angeles: Getty Publications, 2003), 272.
  • John B. Wickstrom: "Text and Image in the Making of a Holy Man: An Illustrated Life of Saint Maurus of Glanfeuil (MS Vat. Lat. 1202)," Studies in Iconography 14(1994), 53-85.
  • Ibid. The Life and Miracles of St. Maurus: Disciple of Benedict, Apostle to France (Kalamazoo, Cistercian Publications, 2008).

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.