Nenda kwa yaliyomo

Msikiti wa Mandhry

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Msikiti wa Mandhry ni msikiti ulioko katika mji wa kale wa Mombasa. Yasemekana ni msikiti mkongwe zaidi mjini humo, [1] na wa pili kwa ukongwe nchini Kenya. Ulijengwa na Waomani mnamo 1570 (977-978 AH), na umekuwa ukitunzwa na ukoo wa Mandhry wa Mombasa kwa karne nyingi. Umejengwa kwa uashi wa kale wa Kiswahili, ukiwa na mnara wa mviringo, na ni mojawapo ya misikiti miwili pekee duniani yenye mihirabu miwili.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Msikiti huo ulijengwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1570 na wahamiaji kutoka Oman. [2] Kulingana na Dkt. Kalandar Khan, ambaye babu yake babu yake alikuwa miongoni mwa wahamiaji wa kwanza. Waswahili waliokuwa kando ya pwani walitafuta msaada kutoka Oman baada ya Wareno kuvamia mji wa Mombasa na kuweka utawala wa kikatili na wa kidikteta ambao Waswahili waliuchukia. Waomani walipofika, walikaa katika eneo la Mji wa Kale, waliijenga nyumba zilokurubuiana. Pia walihitaji mahali pa ibada, jambo lililosababisha kujengwa kwa Msikiti wa Mandhry. [2] Msikiti huo ulipewa jina la ukoo wa Mandhry, ambao ulikaa katika Mji wa Kale, na umetunzwa na ukoo huo kwa karne nyingi. [2]

Msikiti huo umenusurika tangu enzi ya utawala wa Wareno katika maeneo ya pwani.

Msikiti huo ulikarabatiwa mwaka wa 1988. [3]

Uashi na mtindo

[hariri | hariri chanzo]

Msikiti huu umejengwa kwa mtindo wa uashi wa Kiswahili . Ni mmoja kati ya misikiti miwili pekee duniani yenye mihirab mbili (maeneo yanayoonyesha mwelekeo wa msikiti mtakatifu wa Makka ), mwingine ukiwa ni Masjid Qiblatain huko Saudi Arabia. [2]

Awali msikiti huo ulikuwa mweupe, ulijengwa kwa kutumia matumbawe yaliyochomwa na kuwa majivu na kuchanganywa katika kusagwa na chokaa. [2] Licha ya kuibuka kwa madhehebu ya Kiislamu ya Shafi miongoni mwa Waomani kwenye Pwani ya Waswahili katika karne ya 16, Ibadi yao ilikuwa si haba, ambayo inaonyeshwa katika mtindo wa ibadi ya Misikiti ya Wamandhry. [ <span title="This claim needs references to reliable sources. (February 2026)">nukuu inahitajika</span> ] Sehemu ya nje ya msikiti huo haina zaa zaa sana bali ni muondo na muonekano wa kawaida tu, huku sehemu ya ndani ikiwa na milango mitano yalionakishiwa, madirisha manne yaliyochongwa, maandishi, madawati, na nafasi zenye matao. Pia ina mnara wa mviringo, sehemu adhimu inayoshirikiwa na misikiti michache tu kando ya Pwani ya Uswahili. Karibu na hapo kuna kisima cha Mandhry, ambacho kwa kawaida hutumika kwa kutawadhia (udhu). Msikiti huo baadaye ulipakwa rangi ya manjano ili kuuhifadhi na kuutofautisha na majengo yanayouzunguka. [2]

Sehemu ya zamani zaidi ya msikiti, ilijengwa mwaka wa 1570 na awali ilikuwa ikimudu waumini wapatao kumi, ina mionekano kadhaa ya awali. Inahifadhi misahafu (Quran) ya zamani iloandikwa kwa mikono, inayoonekana katika kioo kilobandikwa ndani mwa nguzo za msikiti huo inayodhibitiwa na hali ya hewa, pamoja na minbar ya asili yenye maandishi ya Quran. Ingawa msikiti huo ulipanuliwa yapata karne moja iliyopita, mabaki haya na muundo wa awali wa ndani bado haujaharibika katika hali yake ya mwanzo. [2]

  1. ↑ "Mandhry Mosque | Mombasa, Kenya | Attractions". Lonely Planet. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 1 2 3 4 5 6 7 "Masjid Mandhry Tempat Al-Quran Tertua di Kenya Disimpan". Oase.id (kwa Kiindonesia). 2023-12-03. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2026-07-22. Iliwekwa mnamo 2026-02-19.
  3. ↑ "Archnet > Site > Mandhry Mosque Expansion". www.archnet.org (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2025-08-06. Iliwekwa mnamo 3 Agosti 2025.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)