Msikiti wa Malindi, Zanzibar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Msikiti wa Malindi)
Mnara wa msikiti wa Malindi
Mwonekano wa mbele wa msikiti wa Malindi

Msikiti wa Malindi (pia: Msikiti wa Mnara) ni msikiti uliopo ndani ya Mji Mkongwe, Zanzibar, Tanzania; upo karibu na bandari.[1] Ni mmoja kati ya misikiti kongwe ndani ya Zanzibar, mpaka karne ya 15.[2] Malindi ni jina la sehemu ya Mji Mkongwe.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ulijengwa mnamo mwaka 1834-1835/1250 AH na Muhammad ben Abdulkadir al-Mansaby kutoka pwani ya Benadir katika Somalia ya leo. Katika miaka ya 1820 hadi 1840 huyo alikuwa mfanyabiashara tajiri mjini Zanzibar. Kuna uwezekano mkubwa kwamba msikiti huo ulijengwa kwenye nafasi ya msikiti wa Kisunni uliotangulia kuwepo tangu karne ya 17 au zamani zaidi, lakini habari hii haina uhakika. Msikiti ulipanuliwa mwaka 1841, halafu tena na Seyyid Ali bin Said mnamo 1890[3].

Msikiti una tabia ya pekee ambayo ni mnara wake wenye umbo la pia (moja kati ya minara mitatu ya aina hiyo ndani ya Afrika Mashariki) na jukwaa la mraba.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. (2009) Zanzibar: Pemba, Mafia : the Bardt Travel Guide. Bradt Travel Guides, 177. ISBN 978-1-84162-254-5. Retrieved on 4 April 2013. 
  2. Briggs, Philip (2009). Tanzania: With Zanzibar, Pemba and Mafia. Bradt Travel Guides, 547. ISBN 978-1-84162-288-0. Retrieved on 4 April 2013. 
  3. Mnara Mosque Zanzibar, Tanzania, tovuti ya archnet (elimu ya usanifu wa jamii za Kiislamu ínayoendeshwa na Taasisi ya Agha Khan), iliangaliwa Machi 2021

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

  • Bianca, Stefano & Francesco Siravo. Zanzibar: A Plan for the Historic Stone Town, 41. Geneva: The Aga Khan Trust for Culture, 1996.
  • Finke, Jens. The rough guide to Zanzibar. London: Rough Guides, 2010.
  • Fitzpatrick, Mary, Tim Bewer, and Matthew Firestone. East Africa, 128. Footscray, Vic: Lonely Planet, 2009.
  • Sheriff, Abdul. The History and Conservation of Zanzibar Stone Town, 51. Zanzibar: Department of Archives, Museums and Antiquities, 1995.