Msikiti wa Gaddafi, Dodoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Msikiti wa Gaddafi)

Msikiti wa Gaddafi ndio msikiti mkubwa zaidi nchini Tanzania na wa pili kwa ukubwa Afrika Mashariki baada ya Msikiti wa Kitaifa wa Uganda nchini Uganda. Uko katika mji mkuu wa Tanzania wa Dodoma. Uko katika majira nukta 6°10′22″S 35°44′45″E / 6.172689°S 35.745721°E / -6.172689; 35.745721

Ulipewa jina la Kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi ambaye alitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wake kupitia Jumuiya ya Ulimwengu ya Miito ya Kiislamu. Msikiti huo ulizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2010 na una uwezo wa kuchukua waumini wasiopungua 3,000. [1]

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. MSANGYA (5 March 2011). Gaddafi “gifts” to Tanzania in limbo. africareview.com. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-09-25. Iliwekwa mnamo 6 July 2013.