Moyo Safi wa Maria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Logo ya Moyo Safi.

Moyo Safi wa Maria ni namna Wakatoliki wanavyomheshimu Bikira Maria kwa maisha yake ya Kiroho kama yanavyodokezwa na Luka katika Injili yake. Humo alisisitiza tabia ya Mama wa Yesu ya kuweka na kutafakari moyoni mwake yote yaliyomhusu Mwanae.[1][2]

Kwa kawaida moyo wake unachorwa umechomwa kwa panga saba au una vidonda saba kulingana na mateso yaliyompata kwa ajili ya Yesu.

Heshima kwa moyo wa Maria inaendana na ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu[3].

Kati ya watakatifu waliowahi kuwa na heshima hiyo kuna Anselm wa Canterbury, Bernardo wa Clairvaux, Matilda wa Ringelheim, Gertrudi wa Thuringia na Brigita wa Uswidi.[4]

Baadaye Yohane Eudes (alifariki 1681) alieneza heshima hiyo na kufanya iwe na adhimisho katika kalenda ya liturujia, kwanza huko Autun mwaka 1648 halafu katika majimbo mengine ya Ufaransa. Pia alianzisha mashirika mbalimbali kwa ajili hiyo na kutoa kitabu kikubwa Coeur Admirable (Moyo wa Ajabu, 1681).[5][6]

Hatimaye, mwaka 1805 Papa Pius VII aliruhusu sikukuu ya namna hiyo.[7]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Moyo Safi wa Maria kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.