Nenda kwa yaliyomo

Moutya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Moutya au Moutia, ni ngoma ya kitamaduni ya Kiafrika inayofanana na Sega, lakini mara nyingi huwa na miondoko ya kudokeza. Wachezaji wa kiume na kike husogea kwa mpangilio wa mdundo wa ngoma ambayo mara nyingi hutengenezwa kwa ngozi ya mbuzi iliyokaushwa kabla ya ngoma kuanza. Dansi huanza polepole kulingana na mdundo wa ngoma, huongeza kasi na kuwa na kuwa na hisia za kimahaba zaidi kadiri upigaji wa ngoma unavyokuwa wa haraka zaidi na zaidi.

Pigo na mdundo huambatana na uimbaji.Ambayo kwa kawaida husimulia changamoto na furaha za maisha ya kila siku.Hadi mwishoni mwa miaka ya 1970,Moutya ilichukuliwa kuwa ngoma yenye machocheo ya kimahaba zaidi , na kiujumla iliepukwa[1]

Orodha ya urithi wa kitamaduni usiogusika wa binadamu.

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2019 Shelisheli ilijaribu kuisajili Moutya kama tovuti ya urithi wa kitamaduni usioonekana, lakini ombi lilionekana kama halijakamilika. Hatimaye usajii ulifanyika mwaka 2021 David André, katibu mkuu Shelisheli anaeleza usajili huo kama mafanikio, ambayo yatawezesha kipengele cha kiutamaduni kupitushwa kwa vizazi vijavyo kulingana na maelezo rasmi ya UNESCO Moutya huonyesha utambulisho wa kiutamaduni na huhifadhi vitu vya kiutamaduni inapitishwa kwa njia ya kuiga, nyaraka na utafiti.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-12-11. Iliwekwa mnamo 2026-03-26.