Motlalepula Rosho
Mandhari
Motlalepula Ziphora Rosho (alizaliwa 19 Julai 1970) ni mwanasiasa wa Afrika Kusini na mwanachama wa African National Congress (ANC).
Alichaguliwa mwaka 2010 kuwa Naibu Spika wa Bunge la Mkoa wa North West. Mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Utendaji (MEC) wa Maendeleo ya Uchumi, Mazingira, Uhifadhi na Utalii katika serikali ya mkoa huo.
Mnamo 2014 aliondolewa kwenye baraza la mawaziri la mkoa na baadaye alihudumu kama mwenyekiti wa kamati katika bunge la mkoa hadi Desemba 2018, aliporudi tena serikalini kama MEC wa Serikali za Mitaa na Makazi ya Watu.[1]
Baada ya uchaguzi wa 2019, aliteuliwa kuwa MEC wa Fedha. Kufuatia uchaguzi wa 2024, alichukua nafasi ya Chief Whip wa Bunge la Mkoa..[2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Profile of MEC Motlalepula Rosho". NWDC (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2013-04-25. Iliwekwa mnamo 2021-10-14.
- ↑ "North West Legislature Sworn-in MPLs, Elects Hon. Mohono as New Speaker and Hon. Mokgosi as Premier of North West Province - nwpl" (kwa American English). 2024-06-14. Iliwekwa mnamo 2024-07-08.
| Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Motlalepula Rosho kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |