Nenda kwa yaliyomo

Monoksidi kabonia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Monoksidi kabonia

Monoksidi kabonia (pia: Monoxidi ya kaboni, kwa Kiingereza carbon monoxide) ni kampaundi inayounganisha atomi moja ya oksijeni na atomi moja ya kaboni katika molekuli. Fomula yake ya kikemia ni CO.

Inatokea wakati wa kuchoma kaboni, yaani mata ogania, kama kuna oksijeni kidogo tu; katika mchakato wa kawaida hutokea dioksidi kabonia.

Ni fueli nzuri inaoonyesha miale ya buluu wakati wa kuwaka. Katika hali ya gesi ni sumu kali isiyo na ladha, harufu wala rangi.

Inaweza kusababisha kifo kama moto unawaka katika nyumba au jikoni na watu wanaivuta ndani ya mapafu; inaingia katika damu na kuzuia usafirishaji wa oksijeni katika seli nyekundu za damu.

Monoksidi kabonia ina matumizi mbalimbali ya kiteknolojia, kwa mfano katika uzalishaji wa chuma kutoka mbale kwa sababu inaondoa oksijeni kwenye mbale unaoyeyushwa.

Fomula yake ni

2C + O2 → 2CO

au kwa kupuliza mvuke wa maji katika makaa ya kuwaka

C + H2O → CO + H2

Iliwahi kutumiwa kama fueli ya magari kwa kuchoma vipande vya kuni kwa joto duni na gesi iliweza kuchomwa ndani ya injini ya gari.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Monoksidi kabonia kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.