Nenda kwa yaliyomo

Moncef Dhouib

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Moncef Dhouib (Kiarabu: المنصف ذويب) (alizaliwa mwaka 1952 mjini Sfax) ni mwongozaji wa filamu, mwigizaji, mwandishi wa miswada, mtayarishaji, na mchezeshaji wa vikaragosi kutoka nchini Tunisia. Yeye ni mshindi wa tuzo ya FESPACO. Baada ya kutengeneza filamu fupi nne zilizopata umaarufu mkubwa katika miaka ya 1980, alitengeneza filamu za The Sultan of the City (Soltane El Medina) (1993) na The TV arrives (Talfaza Jaya) (2006).[1]

Alisoma katika Chuo Kikuu cha Paris.[2]

Aliandaa maonyesho makubwa ya chezeshaji wa vikaragosi.[3]

Mnamo mwaka 2014, aliandika kitabu kilichoitwa Le roi et les trois buffles.[4]

Filamu zilizochaguliwa

[hariri | hariri chanzo]

Muigizaji

Aliigiza nafasi ya mjakazi mnamo 1983 katika filamu ya Misunderstood.

Uongozaji Filamu

Aliongoza mfululizo wa filamu fupi mnamo 1980.

  • 1986: Hammam D'hab iliyoandikwa na Hedi Abassi.
  • 1989: El hadhra.
  • 1992: Soltane El Medina (The Sultan of The City) iliyoongozwa na Ahmed Baha.
  • 1995: Tourba.
  • 1999: Les siestes grenadine (Grenadine naps) iliyoongozwa na Mahmoud Ben Mahmoud.
  • 2006: Alitayarisha na kuongoza filamu ya vichekesho iitwayo Talfaza Jaya iliyotengenezwa na kampuni ya Manara Productions.

Ukumbi wa Maigizo

Pia aliandika maonyesho matatu yaliyopata mafanikio makubwa nchini Tunisia:

  • 1993: Makki and Zakia na Fi hak Essardouk Enraychou (michezo ya kuigiza ya mtu mmoja) iliyoigizwa na Lamine Nahdi (kila mmoja kati ya michezo hiyo alitumbuiza kwa zaidi ya miaka sita).
  • 2008: Mme Kenza lililoigizwa na Wajiha Jendoubi.
  • Manseya Fe Al Entekhabet Al Re2aseya (Aliyesahaulika kwenye Uchaguzi wa Rais) lililotumbuizwa na Naima El Jeni.

Alipokea Tuzo ya Filamu Fupi Bora katika Tamasha la 7 la Filamu za Afrika mjini Milan, Italia.

  1. Armes, Roy (2008-07-11). Dictionary of African Filmmakers (kwa Kiingereza). Indiana University Press. ISBN 978-0-253-35116-6.
  2. "Personnes | Africultures : Dhouib Moncef". Africultures (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2026-05-26.
  3. "Africiné - Moncef Dhouib". Africiné (kwa Kifaransa). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-12-11. Iliwekwa mnamo 2026-05-26.
  4. Editions Seuil Jeunesse. "Le lion et les trois buffles aux éditions Seuil Jeunesse". seuiljeunesse.com (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2026-05-26.