Nenda kwa yaliyomo

Mohammed Abdel Wahab

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mohammed Abdel Wahab

Mohammed Abdel Wahab (Kiarabu:محمد عبد الوهاب, Mohamed Abd El-Wahhab (Machi 13, 1902 - Mei 4, 1991) alikuwa ni mwimbaji, mwigizaji na mtunzi maarufu wa nchini Misri aliyeishi katika karne ya 20. Anafahamika zaidi kwa nyimbo zake za kimapenzi pamoja na nyimbo zake za lugha ya kimisri.

Alifahamika kwa nyimbo zake za kizalendo na Mapinduzi kama "Ya Masr tam El-Hanna" (Oh Misri, furaha ipo hapa), "Hay Ala El-Falah" (Mwito wa wajibu), "El Watan El Akbar", "Masr Nadetna falbena El-neda", "Oulo le Masr" (Mwambie Misri), "Hob El-watan Fard Alyi", "Sout El-Gamaheer", "Ya Nessmet El-Horria" , "Sawae'd watu Beladi".

Pia alichangia na kutengeneza nyimbo za taifa za Tunisia, "Humat al-Hima", Umoja wa Falme za Kiarabu, "Īsiy Bilādis", na "Libya" kuanzia mwaka 1951 hadi 1969.

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mohammed Abdel Wahab kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.