Nenda kwa yaliyomo

Mohamed Juldeh Jalloh

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mohamed Juldeh Jalloh (alizaliwa 1970) ni mwanasiasa wa Sierra Leone na makamu wa rais wa Sierra Leone tangu 4 Aprili 2018. Jalloh ni mwanafalsafa wa siasa, mfanyabiashara, na aliyewahi kuwa afisa wa Umoja wa Mataifa. Pia ni mwanachama mwandamizi wa Sierra Leone People's Party.

Jalloh alihitimu na shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa kutoka Fourah Bay College, alisoma shahada ya uzamili ya sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha University of Ibadan huko Ibadan, Nigeria; na shahada ya udaktari katika chuo cha University of Bordeaux huko Bordeaux, Ufaransa.[1] Anaongea lugha kadhaa ikiwa ni pamoja na Kiingereza na Kifaransa.

Kitaaluma, Jalloh alianza kazi yake na Umoja wa Mataifa mwaka 2000, akiwa afisa wa programu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo. Pia amewahi kuwa mwanachama wa bodi ya washauri wa ngazi ya juu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuimarisha amani nchini Mali na katika kanda ya Sahel.

  1. "SLPP Mohamed Juldeh Jalloh Has A Track Record Of Achievements". SLPP Today. 17 Januari 2018.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mohamed Juldeh Jalloh kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.