Mofolojia (isimu)
Mofolojia (kutoka maneno ya Kigiriki morphe, umbo, na logos, neno; pia: sarufi maumbo) ni tawi la isimu ambalo huchunguza maneno ya lugha fulani na aina zake za maneno, hasa upande wa upangaji wa mofimu mbalimbali zitumikazo kwa ajili ya kuunda maneno.
Mofolojia ni taaluma ya isimu ambayo inachunguza maumbo ya maneno ama maneno kamili yanayobeba maana, ikijumuisha kanuni ambazo kwayo huundwa, na jinsi yanavyohusiana katika lugha . [1] [2].
Maumbo ya maneno ni matokeo ya muunganiko wa fonimu mbalimbali ambazo pia huungana na kuunda - hatimaye na kuwa neno. Yaani, Fonimu ---> Silabi ---> Neno.
Mbinu nyingi za mofolojia huchunguza muundo wa maneno kwa mujibu wa mofimu, ambazo ni vipashio vidogo zaidi katika lugha yenye maana fulani huru. Mofimu ni pamoja na mizizi ambayo inaweza kuwepo kama maneno yenyewe, lakini pia kategoria kama vile viambishi ambavyo vinaweza kuonekana tu kama sehemu ya neno kubwa. Kwa mfano, katika Kiingereza, mzizi catch na kiambishi tamati -ing zote ni mofimu; catch inaweza kuonekana kama neno lake yenyewe, au inaweza kuunganishwa na -ing kuunda neno jipya catching . Mofolojia pia huhusika na uchanganuzi wa jinsi maneno yanavyoweza kubadilika katika aina mbalimbali za maneno, na jinsi yanavyoweza kubadilika kueleza kategoria za kisarufi ikiwamoi namba, wakati na kipengele. Dhana kama vile tija inahusika na jinsi wazungumzaji wanavyounda maneno katika miktadha maalumu, ambayo hubadilika kulingana na historia ya lugha.
Nyanja za msingi za isimu huzingatia kwa mapana muundo wa lugha katika "mizani" tofauti. Mofolojia inachukuliwa kufanya kazi kwa kiwango kikubwa kuliko fonolojia, ambayo huchunguza kategoria za sauti za usemi ambazo hutofautishwa ndani ya lugha inayozungumzwa, na hivyo inaweza kujumuisha tofauti kati ya mofimu na nyingine. Kinyume chake, sintaksia inahusika na kiwango kinachofuata kwa ukubwa, na huchunguza jinsi maneno kwa upande wake huunda vishazi na sentensi. Taipolojia ya kimofolojia ni fani tofauti inayoainisha lugha kulingana na sifa za kimofolojia zinazoonyeshwa.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Anderson, Stephen R. (n.d.). "Morphology". Encyclopedia of Cognitive Science. Macmillan Reference, Ltd., Yale University. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2016.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Aronoff, Mark; Fudeman, Kirsten (n.d.). "Morphology and Morphological Analysis" (PDF). What is Morphology?. Blackwell Publishing. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 27 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 30 Julai 2016.
{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
- Habwe J. na Karanja P. 2004, "Misingi ya Sarufi ya Kiswahili"
| Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mofolojia (isimu) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |