Mnyama Ngozi-miiba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mnyama ngozi-miiba
Shashile katika Kenya (Diadema setosum)
Shashile katika Kenya (Diadema setosum)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia
Nusuhimaya: Eumetazoa
Faila ya juu: Deuterostoma
Faila: Echinodermata
Ngazi za chini

Nusufaila na ngeli:

Wanyama ngozi-miiba (kutoka Kiholanzi stekelhuidigen) ni wanyama wa bahari ambao wana ngozi yenye miiba na ulinganifu wa pembetano ingawa wahenga wao walikuwa na uwenzipacha. Hata lava wao wana uwenzipacha lakini hukuza pande tano wakiwa wazima. Mifano ya wanyama ngozi-miiba ni viti vya pweza, changa-maji, shashile, chani na kojojo.

Mwili wa wanyama ngozi-miiba una pande tano na umefunikika kwa ngozi yenye fuwele za kalsiti (kabonati ya kalisi) ziitwazo ossicles (vifupa). Kwa hivyo wanyama hawa wana aina ya kiunzi cha nje. Vifupa vya kiunzi hicho vimeunganika kabisa, kama kwa shashile na jamaa, au vimeunga kwa viungo, kama kwa viti vya pweza, changa-maji na kojojo. Katika matukio mengi vifupa hivyo vina michomozo kwa umbo la miiba, sugu au chembe (asili ya jina la faila hii).

Vineli vidogo vichomoza kupitia nyeleo za kiunzi. Kwa wanyama ngozi-miiba wengi hivi vinaweza kutumika kwa kusogea. Kwa wengine, kama mileli-bahari, hutumika kwa kukamata mawindo tu. Miguu hii ya neli (tube feet) inaweza kujishikiza chini au kwenye mawindo kwa njia ya mfyonzo.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu "Mnyama Ngozi-miiba" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asili stekelhuidige kutoka lugha ya Kiholanzi. Neno (au maneno) la jaribio ni mnyama ngozi-miiba.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mnyama Ngozi-miiba kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.