Mnara wa taa wa Benghazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mnara wa taa wa Benghazi

Mnara wa Taa wa Benghazi ni mnara wa taa unaotumika na unapatikana katika pwani ya nchini Libya ndani ya kitongoji cha eneo la Sidi Khrebish huko Benghazi .[1] Namba yake ya NGA ni 21508

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mnara huu wa taa ulijengwa mnamo mwaka 1922 wakati wa ukoloni wa Italia huko Libya na ulizinduliwa mnamo mwaka 1928, ni moja wapo ya alama za zamani na maarufu za kihistoria za Benghazi. Pamoja na kuongoza meli, ulitumika pia kama mnara wa maji.

Mnara huu wa taa unaurefu wa mita 22 (72 futi) naurefu wamita 41 (135 futi). Taa hii inaanuwai ya 17 (nautical mile ).[1]

Mnara wa taa ulipata uharibifu wakati wa Vita vya dunia vya pili, lakini uliharibiwa vibaya zaidi hivi karibuni katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Libya. Baadhi ya wapinzani (Waisilamu) wa kamanda wa jeshi Khalifa Hafter walijificha katika mnara wa taa, na baadaye walitumia kuzika wafu wao karibia 200 . Mashambulio ya angani yaligonga chumba cha juu na kuitoa taa iliyoanguka lakini haikuharibiwa.

Mnamo mwaka 2014, saa ya kipenyo cha mita 5 katika rangi ya bendera ya kitaifa iliingizwa upande wa baharini wa taa, mchango kutoka kwa mfanyabiashara Abubakr Sheikh,[2] licha ya upinzani kutoka kwa jamii ya usanifu.[3]

Ukarabati[hariri | hariri chanzo]

Mradi wa ukarabati uliotangazwa mnamo mwaka 2019 ulikusudia kurudisha mnara wa taa katika hali yake ya asili, na ulikadiriwa kuchukua miezi 13 hadi 17. Mradi huo ulianzishwa na kufadhiliwa na mamlaka ya mitaa ya Benghazi, ambayo ni sehemu ya serikali ya mpito ya mashariki ya Libya, inayoongozwa na Abdullah al-Thinni.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]