Mmea

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 11:19, 7 Desemba 2016 na Kipala (majadiliano | michango)
Mimea

Mimea ni moja ya kundi la viumbe hai duniani ikijumuisha miti, maua, mitishamba,n.k. Kuna zaidi ya aina 300,000 ya mimea.

Sayansi inayochunguza mimea huitwa botania ambayo ni kitengo cha biolojia. Kwenye uainishaji wa kisayansi mimea hujumlishwa katika himaya ya planta kwenye milki ya Eukaryota (viumbehai vyenye kiini cha seli na utando wa seli.).

Kwa hiyo mimea huwa na utando wa seli mwenye selulosi. Mmea unapata sehemu kubwa ya nishati kutoka kwa nuru ya jua kwa njia ya usanisinuru yaani hujilisha kwa msaada wa nuru. Ndani ya majani ya mimea kuna klorofili, dutu kijani, inayofanya kazi ya kupokea nuru na kupitisha nishati yake kwa sehemu nyingine ya mmea ambako inatumiwa kujenga molekuli zinazotunza nishati kwa njia ya kikemia na kutumiwa katika metaboli ya mwili.

Mimea kadhaa imepoteza uwezo wa kutengeneza klorofili ya kutosha hivyo inajipatia nishati yao kama vimelea kutoka kwa mimea au viumbehai vingine.

Mimea mingi inazaa ka njia ya kijinsia yaani kwa kuunganisha seli za kiume na kike; mara nyingi viungo vya kiume na kike vinapatikana ndani ya mmea mmoja. Kuna pia mimea inayozaa kwa njia isiyo ya kijinsia kwa mfano kwa kuotesha mzizi wa hewani unaingia ardhini na kuendelea kama mmea wa pekee.

Mimea ni msingi muhimu kwa viumbehai wengine duniani kwa sababu sehemu kubwa ya oksijeni katika angahewa ya dunia inatengenezwa na mimea.[1]. Mimea inatoa chakula cha kibinadamu kama vile nafaka, matunda na mboga majani, pia lishe kwa wanyama wa kufugwa.

Album

Makala hii kuhusu mmea fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mmea kama uainishaji wake wa kibiolojia, uenezi au matumizi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Field, C.B.; Behrenfeld, M.J.; Randerson, J.T.; Falkowski, P. (1998). "Primary production of the biosphere: Integrating terrestrial and oceanic components". Science 281 (5374): 237–240. Bibcode:1998Sci...281..237F. PMID 9657713. doi:10.1126/science.281.5374.237.