Nenda kwa yaliyomo

Mkuzi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkuzi ni kata ya Wilaya ya Muheza katika Mkoa wa Tanga, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 8,785 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,948 [2]

Msimbo wa posta ni 21419.

Wenyeji wa kata ya Mkuzi ni Wabondei. Asilimia kubwa ya Wabondei ni wakulima wa machungwa, mahindi, mpunga na ndizi, pia wanafuga mbuzi, kuku, bata na ng'ombe wa maziwa.

Kata ya Mkuzi ina vijiji vinne ambavyo ni Mkuzi, Mafere, Mindu na Lunguza. Inasemekana kata ilianzia kwenye kijiji cha Mafere wakati wa biashara ya utumwa. Baadhi ya watumwa waliokuwa dhaifu sana waliachwa hapo na baadaye walipona na kuendelea na maisha hapo. Ikumbukwe kuwa hapo Mafere ndipo ilipopita njia ya kusafirisha watumwa kwenda wilaya ya Pangani ambapo watumwa walisafirishwa kwa njia ya maji kwenda maeneo mengine.

Jina la Mkuzi lilikuwepo tangu zamani za ukoloni wa Wajerumani na ndio waliojenga kanisa kubwa kuliko yote katika kata hiyo. Kanisa hilo lilijengwa kwa kutumia mawe makubwa na bado linatumika kwa ibada, halina ufa wowote.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Tanga Region - Muheza District Council" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-05. Iliwekwa mnamo 2016-04-29.
Kata za Wilaya ya Muheza - Mkoa wa Tanga - Tanzania

Amani | Bwembwera | Genge | Kicheba | Kigombe | Kilulu | Kisiwani | Kwabada | Kwafungo | Kwakifua | Kwemingoji | Kwemkabala | Kwezitu | Lusanga | Magila | Magoroto | Majengo | Makole | Masuguru | Mbaramo | Mbomole | Mhamba | Misalai | Misozwe | Mkuzi | Mlingano | Mpapayu | Mtindiro | Ngomeni | Nkumba | Pande Darajani | Potwe | Songa | Tanganyika | Tingeni | Tongwe | Zirai

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tanga bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkuzi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.