Mkunjo (jiolojia)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mikunjo katika mwamba huko Krete, Ugiriki.
Usawazishaji wa upinde wa mvua karibu na Barstow, California, Marekani.

Mkunjo (kwa Kiingereza: fold) kwa maana ya jiolojia unatokea pale ambako tabaka la mwamba lililokaa kibapa linaathiriwa na miendo katika ganda la Dunia na kupindwa kutokana na shinikizo na jotoridi kubwa. Kwa kawaida sababu ni miendo ya gandunia yaani pale ambako mabamba (vipande vya ganda la Dunia) husukumana.

Mikunjo hutokea mara nyingi katika matabaka ya mwamba mashapo lakini inatokea pia katika miamba ya volkeno.

Kiwango cha kukunjwa hutofautiana kwa ukubwa kuanzia mikunjo midogo sana inayotambuliwa katika hadubini tu, hadi kutokea kwa safu za milima zinazoweza kuitwa milima kunjamano kama vile Himalaya, Alpi, Andes au Rocky Mountains.

Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkunjo (jiolojia) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.