Mkubayoka
Mandhari
Mkubayoka | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 6:
|
Wakubayoka ni spishi za nyoka wasio na sumu za jenasi Natriciteres katika familia Colubridae. Wamepewa jina hili kwa sababu hufikiriwa kuwa feli mbaya (ukuba).
Nyoka hawa ni wafupi. Majike ya spishi kadhaa yanaweza kufika sm 54 lakini madume ni wafupi zaidi na urefu wa wastani ni kati ya sm 20 na 35. Kichwa chao ni kidogo. Rangi yao kijani, kijani-zeituni, kahawia-zeituni, kijivu au takriban nyeusi. Mara nyingi kuna mlia mpana mgongoni wenye rangi kali au angalau rangi isiyoiva.
Wakubayoka huishi karibu na maji na hula vyura na [[samaki] wadogo.
Nyoka hawa hawana sumu na kwa hivyo wanaweza kukamatwa bila hatari.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Natriciteres bipostocularis, Mkubayoka Kusi-magharibi (Southwestern forest marsh snake)
- Natriciteres fuliginoides, Mkubayoka Mkufu (Collared marsh snake)
- Natriciteres olivacea, Mkubayoka Zeituni (Olive marsh snake)
- Natriciteres pembana, Mkubayoka wa Pemba (Pemba marsh snake)
- Natriciteres sylvatica, Mkubayoka-misitu (Forest marsh snake)
- Natriciteres variegata, Mkubayoka Aina-aina (Variable marsh snake)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkubayoka kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |