Mkongo (Rufiji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mkongo ni kata ya Wilaya ya Rufiji katika Mkoa wa Pwani, Tanzania yenye postikodi namba 61604 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,619 [2] walioishi humo.Kijiji cha Mkongo kilianzishwa mwaka 1961.Kabla ya hapo wanakijiji hao waliishi ktk eneo la Lusende kwa sasa hufanywa mashamba ya watu Wa Mkongo.Lusende ipo km4 kutoka Mkongo mjini pia km4 kutoka Mto Rufiji.Asili ya Jina,baada ya uhuru kulianzishwa vijiji vya ujamaa ndipo watu walitoka Lusende na kuhamia Mkongo ambapo kulikuwa na miti mingi aina ya mikongo pia kulikuwa na Mkongo mkubwa Sana ambao ndio ulio beba jina la kijiji na mpaka sasa uwo mti upo tkt Barabara ya kuelekea Lusende(Mashambani) nihiyo barabara inaitwa Mkongo road.Hapo Mwanzo Mkongo ndio kulikua na mji kubwa katika Wilaya ya Rufiji hata Mwalimu JK Nyerere alifika hapo alifikia kwa mzee ALLY MAMBA aliyekuwa mtu Wa kwanza kujiunga na chama cha mapinduzi ktk Wilaya ya Rufiji mwaka 1977,Nerere aliwezesha kujenga Bunge Dogo,Benki,Mahakama ya wilaya,pia kulikuwa na karakana ambayo iliuliwa na kufanywa Shule ya Sekondary itwayo Mkongo mnamo mwaka 1996 pia Kuna Shule za msingi Mbili ambazo ni Mkongo ilijengwa 19961na Kaunda 1976. Mkongo ndipo iliopo Makao makuu ya (RUBADA) Rufiji Basin Development Authority.Wanakijiji wake ni wakabila la Wandengereko Koo zipatikanazo ni Mbonde,Mkumba,Rwambo,Msumi,Mlinda nk.pia ujishughurishs Sana na kulimo cha Mpunga na Mahindi.lakini pia mtu wa kwanza kuugua UKIMWI ktk wilaya ya Rufiji Alitokea Mkongo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Flag of Tanzania.svg Kata za Wilaya ya Rufiji - Mkoa wa Pwani - Tanzania Flag of Tanzania.svg

Bungu | Chemchem | Chumbi | Dimani | Ikwiriri | Kibiti | Kiongoroni | Kipugira | Mahege | Maparoni | Mbuchi | Mbwara | Mchukwi | Mgomba | Mjawa | Mkongo | Mlanzi | Mohoro | Msala | Mtawanya | Mtunda | Mwambao | Mwaseni | Ngarambe | Ngorongo | Ruaruke | Salale | Umwe | Utete


Flag-map of Tanzania.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkongo (Rufiji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.