Mkamzee Mwatela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mkamzee Chao Mwatela (amezaliwa 1982) ni mkurugenzi, mwandishi na muigizaji nchini Kenya, ni maarufu kwa majukumu yake katika safu ya Runinga ya Mali na Stay.[1][2][3]

Mkamzee alisoma shule ya msingi ya Nairobi.Baadae alijiunga na shule maarufu ya wasichana ya Moi Nairobi kwa masomo yake ya sekondari na baadae kwenda Saint Mary's kwa mpango wa kimataifa wa Baccalaureate. Alibobea katika sanaa ya ukumbi wa michezo.

Baada ya miaka mitatu jukwaani (2003 hadi 2006), mwishowe alijiunga na chuo kikuu cha Jimbo la New York huko Buffalo kusoma filamu na ukumbi wa michezo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkamzee Mwatela kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.