Minciu Sodas

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Minciu Sodas ni maabara ya kiteknolojia inayoendeshwa kwa njia ya intaneti yenye lengo la kuunganisha watu, vikundi na hata makampuni kwa kulenga mitazamo yao na michango yao katika jamii. Maabara hii huwahusishwa vijana, wamama, walemavu, wakulima na watu wengine wenye nia ya kutafakari masuala mbalimbali ya kijamii, kisiasa, uchumi pamoja na mambo yahusuyo mabadiliko ya teknolojia.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Minciu Sodas ilianzishwa rasmi mwaka 1998 na Andrius Kulikauska raia wa Lithuania inayopatikana barani ulaya. Maabara hii ilianzishwa kwa lengo la kushirikiana kimawazo baina ya wanachama na jamii. hivyo vilianzishwa vikundi mbalimbali ambavyo vililenga kuwaunganisha wanachama wenye mitazmo inayolingana.

Makundi ya wanachama[hariri | hariri chanzo]

Vikundi vya wanachama ni vikundi vinavyolenga watu wenye mitazamo inayoendana. Mfano wanachama wanaopenda maswala yanoyohusu tekinolojia ya kompyuta hushirikiana kwa kikundi kilichopewa jina la "jifunze namna ya kujifunza" (learnhowtolearn). Vikundi vingine ni kama Hakielimu kinachojihusisha na maswala ya maendeleo ya elimu kinachoendeshwa na kikundi cha Uyoga, Learning from each other (Jifunze kwa pamoja), National Treasure (rasilimali za nchi na vikundi vinginevyo.

Jinsi ya kushiriki[hariri | hariri chanzo]

Unaweza kushinikiana na maabara hii ya wanaharakati kwa kubadilishana jumbu kwenye chumba cha mawasiliiano hapa au kujiunga na moja kati ya viikundi vilivyo anzishwa na kuweza kushirikiana na wanachama walioko kwenye kundi husika.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Minciu Sodas kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.