Millot Abena Pokuaa
Mandhari
Millot Abena Pokuaa (alizaliwa10 Oktoba, 2001) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa wanawake wa kitaalamu kutoka nchini Ghana anayekipiga kama mshambuliaji katika klabu ya mpira ya Hasaacas Ladies inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Ghana, pamoja na timu ya taifa ya wanawake ya Ghana.
Aliiwakilisha Ghana katika ngazi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 katika Michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Pokuaa alijiunga na klabu ya Hasaacas Ladies mwaka 2019.[1]
Mwaka 2020, alichaguliwa kwa mara ya kwanza kujiunga na timu ya taifa ya wanawake ya Ghana kwa ajili ya Michuano ya Kufuzu ya Olimpiki ya Wanawake ya CAF ya mwaka 2020.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Millot Pokuaa - Soccer player profile & career statistics - Global Sports Archive". globalsportsarchive.com. Iliwekwa mnamo 2021-08-04.
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Millot Abena Pokuaa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |