Milipuko ya mwaka 2011 jijini Dar es Salaam
Milipuko ya mwaka 2011 jiini Dar es Salaam ilikuwa mfululizo wa milipuko ya mabomu katika ghala la kuhifadhia silaha katika kata ya Gongolamboto Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Tanzania, ambayo yaliua watu 20-32.[1] Kulingana na maafisa wa kituo hicho, mlipuko wa kwanza ulitokea saa 2:30 usiku kwa saa za Afika mashariki ukiwa ni mlipuko wa pili katika miaka miwili ya ghala la silaha karibu na makazi ya watu wengi, vikundi kadhaa vilihoji maeneo ya vituo hivi vya kuhifadhi silaha na kuomba vihamishwe. Ripoti zinaonyesha kwamba majengo 23 ya kijeshi, nyumba mbili na shule ziliharibiwa.[2]
Mlipuko wa kwanza kati ya kadhaa ulioripotiwa ulitokea majira ya saa 4 usiku kwa saa za Afrika Mashariki, mashuhuda waliripoti kwamba milipuko iliendelea mara kwa mara katika kipindi cha takribani saa moja iliyofuata.[3] Ripoti za vyombo vya habari zilisema kuwa kati ya watu 20 na 32 waliuawa na milipuko hiyo [1] na wengine 300 walijeruhiwa huku nyumba zikibomolewa na vifusi vikianguka kutoka angani. Vifo vilitokana na milipuko hiyo moja kwa moja au matokeo ya shinikizo la damu.[1] Uchafu wa vifusi uliripotiwa umbali wa kilomita 15 kutoka kambini . Takriban watoto 200 waliripotiwa kukosa wazazi wao pia; haikujulikana ikiwa wazazi wao hawakupatikana kutokana na milipuko hiyo au walitenganishwa wakati wa kuhamishwa.[4]
Mara tu kufuatia tukio hilo, ma afisa katika jiji hilo waliwaamuru wakazi wote waliokuwa ndani ya eneo la kilomita 10 kutoka kambi ya kijeshi kuhama.[3] Wakazi wanaokadiriwa kufikia 4,000 walikimbia nyumba zao.[4] Wakaazi wa jiji hilo walitoa wito kwa waziri ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Hussein Mwinyi, na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange kujiuzulu. Mnamo Februari 17, uchunguzi ulianzishwa ili kupata sababu ya milipuko hiyo.
Uwanja mkuu wa ndege nchini, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, pia ulifungwa kwa muda.[5] Tukio kama hilo lilitokea Aprili mwaka 2009 katika kata ya Mbagala jijini.[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- 1 2 3 "Home". www.ippmedia.com. Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- ↑ "Vatican Radio - Explosion causes mayhem in Tanzania". www.oecumene.radiovaticana.org (kwa Kiitaliano). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-27. Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- 1 2 Monica Sarkar. "Breaking News, Latest News and Videos". CNN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-10-06.
- 1 2 25 killed in Tanzania blasts after accidental explosion at military base in capital city, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-07-07, iliwekwa mnamo 2025-10-06
- ↑ "Tanzania blasts: At least 20 dead in Dar es Salaam", BBC News (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2011-02-17, iliwekwa mnamo 2025-10-06
- ↑ Deadly blasts rock Tanzanian city (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2009-04-29, iliwekwa mnamo 2025-10-06