Nenda kwa yaliyomo

Mikhail Lobukhin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mikhail Lobukhin ni mcheza dansi mkuu wa Baleti ya Bolshoi wa Urusi.

Alizaliwa katika mji wa Saint Petersburg, Urusi. Mnamo mwaka 2002 alihitimu kutoka Vaganova Ballet Academy akiwa na shahada ya sanaa na katika mwaka huo huo alijiunga na Tamasha la Marinsky. Miaka minane baadaye alijiunga na Baleti ya Bolshoi ambapo alicheza nafasi nyingi za solo lakini pia alionekana kama kijana katika Leningrad Symphony, prince katika Cinderella, Daphnis katika Daphnis and Chloe, na Ivan the Fool katika Little Humpbacked Horse miongoni mwa wengine. Mwaka 2010 alionekana kama Basilio katika Don Quixote iliyotolewa katika Novosibirsk State Academic Opera and Ballet Theatre na mwaka uliofuata alicheza kama Bahram Shah katika Seven Beauties katika Azerbaijan State Academic Opera and Ballet Theatre.[1]

  1. "Mikhail Lobukhin". Baleti ya Bolshoi. Iliwekwa mnamo Oktoba 10, 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mikhail Lobukhin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.