Mika Yamamoto
Mika Yamamoto (26 Mei 1967 – 20 Agosti 2012) alikuwa mwandishi wa habari wa video na picha wa Japani aliyepewa tuzo, akifanya kazi katika shirika la habari la Japan Press.Yamamoto aliuwawa mnamo 20 Agosti 2012 akiwa anafuatilia Vita vya Ndani vya Syria huko Aleppo, Syria. Alikuwa wa kwanza wa Japani na mwandishi wa habari wa kigeni wa nne kuuawa katika Vita vya Ndani vya Syria vilivyoanza mnamo Machi 2011. Alikuwa mwandishi wa kumi na tano kuuawa nchini Syria mwaka 2012.
Asili ya Familia
[hariri | hariri chanzo]Yamamoto alizaliwa huko Tsuru, Yamanashi, mji ulioko katika Jimbo la Yamanashi, mnamo 26 Mei 1967.Alikuwa na dada wawilina baba yake, Koji Yamamoto, ni mwandishi wa zamani wa Asahi Shimbun.
Kazi katika Uandishi wa Habari
[hariri | hariri chanzo]Yamamoto alianza kazi yake mwaka 1990 kama mwandishi wa habari wa Asahi Newstar, katika kituo cha runinga ya satelaiti cha TV Asahi, na hatimaye akawa mwandishi wa video na mkurugenzi wa nyaraka na programu za habari.[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Shigeki Tao (22 Agosti 2012). "Japanese shot dead in Syria". Daily Yomiuri. Cairo. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2012.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Siria, uccisa giornalista Mika Yamamoto vincitrice del Pulitzer giapponese". Il Messaggero. 21 Agosti 2012. Iliwekwa mnamo 21 Agosti 2012.
{{cite news}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mika Yamamoto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |