Miguel La Fay Bardi
Mandhari
Miguel La Fay Bardi, O. Carm., (Chelsea, Massachusetts, 11 Novemba 1934 – Boston, Massachusetts, 20 Oktoba 2021) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki mwenye asili ya Marekani.
La Fay Bardi alihudumu kama Mkuu wa kanda ya Kikanisa ya Sicuani, ambayo sasa inajulikana kama Dayosisi ya Kanisa Katoliki ya Sicuani nchini Peru, kuanzia tarehe 26 Julai 1999 hadi alipostaafu tarehe 10 Julai 2013.
Alipadrishwa katika Shirika la Wakarmeli tarehe 4 Julai 1960.
Askofu mstaafu Miguel La Fay Bardi alifariki akiwa na umri wa miaka 86.[1][2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Bishop Miguel La Fay Bardi O. Carm". Order of the Carmelites. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-24. Iliwekwa mnamo 2021-11-21.
- ↑ "Cusco: fallece monseñor Miguel La Fay Bardi O. Carm, obispo emérito de la diócesis de Sicuani". La República. 2021-10-20. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-08-24. Iliwekwa mnamo 2021-11-22.
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |