Mhandisi mwanateknolojia
Mhandisi mwanateknolojia ni mtaalamu wa uhandisi aliyefunzwa katika nyanja fulani za ubunifu, upangaji na utekelezaji wa eneo husika la teknolojia ya uhandisi. Elimu ya teknolojia ya uhandisi huzingatia zaidi matumizi zaidi, kuliko elimu ya sayansi ya uhandisi . Kwa kawaida, wahandisi wanateknolojia huwa wasaidizi wa wahandisi.
Ufafanuzi
[hariri | hariri chanzo]Wahandisi wanateknolojia huusika zaidi kuliko wahandisi wengine katika kuzingatia utekelezaji wa baada ya upangaji, utengenezaji wa bidhaa, au uendeshaji wa teknolojia. Wanahusishwa kutekeleza mipango iliyobuniwa na mhandisi.
Sheria ya Teknolojia ya Uhandisi ya Kenya inaelezea mhandisi mwanateknolojia kuwa ni mtu anayetoa huduma ambayo inahitaji, au inategemea, matumizi ya kanuni na takwimu za uhandisi katika shughuli za maendeleo, utekelezaji, ujenzi na uzalishaji zinazohusiana na teknolojia ya uhandisi, na ambayo haihusishi huduma ya uhandisi inayotolewa kwa mujibu wa kiwango cha kimaelekezo pekee. Pia anaweza kufanya kazi zinazojumuisha huduma za kitaalamu, ushauri, uchunguzi, tathmini, upangaji, usanifu au jukumu la usimamizi wa ujenzi, uendeshaji au matengenezo kuhusiana na huduma za umma zinazomilikiwa na serikali au sekta binafsi, majengo, mashine, vifaa, michakato, kazi au miradi ambayo utekelezaji wake unahitaji matumizi ya kanuni na takwimu za uhandisi[1].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Engineering Technology Act (kwa Kiingereza). 2022-12-31.