Mgongo wa bahari ya Pasifiki-Antaktiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mgongo wa bahari ya Pasifiki-Antaktiki inaonekana katika sehemu ya chini ya picha, juu yake mgongo wa bahari ya Pasifiki Mashariki na mgongo wa bahari ya Chile.

Mgongo wa bahari ya Pasifiki-Antaktiki ni mgongo kati wa bahari katika Bahari ya Pasifiki ya kusini na pia kwenye Bahari ya Kusini. Ni kama safu ya milima ya volkeno kwenye sakafu ya bahari.

Unatenganisha Bamba la Pasifiki na Bamba la Antaktiki[1]. Mabamba hayo ya gandunia yanaachana kwa kasi ya milimita 54 na 76 kwa mwaka[2]. Kwenye mstari yanapoachana kuna ufa ambako magma moto kutoka koti ya Dunia inapanda juu ikiingia katika maji ya bahari ambako inapoa na kuganda. Kwa njia hiyo magma ikipoa inajenga safu ya milima.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Pacific-Antarctic-Ridge, tovuti ya Britannica, iliangaliwa Novemba 2019
  2. Hélène Ondréas, Daniel Aslanian: Variations in axial morphology, segmentation, and seafloor roughness along the Pacific-Antarctic Ridge between 56°S and 66°S. In: Journal of Geophysical Research 106:B5, 2001, pp. 8521–8546, doi:10.1029/2000JB900394

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]