Mgogoro wa kimazingira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Migogoro ya kimazingira hupatikana katika sehemu mbalimbali kama kwenye madini,uchafu,nakadhalika

Mgogoro wa kimazingira (kwa Kiingereza: Environmental conflict) ni mgogoro unaosababishwa na uharibifu wa mazingira kwenye masuala ya kushindwa kusimamia rasilimali za mazingira.[1]

Mara nyingi pande tofauti zinahusishwa ikiwemo watetezi wa mazingira ambao wanataka kulinda mazingira na watu au makampuni yanayolenga kutumia maliasili bila kujali athari hasi kwa mazingira mfano migodi ya madini.[2] Athari hasi hutokea pamoja na kuachia kemikali za sumu hewani au majini, kukata miti mingi, matumizi ya maji mengi mno, kusababisha machafuko ya aina mbalimbali, kuhatarisha ekolojia ya eneo husika.[3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]