Nenda kwa yaliyomo

Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo (kwa Kiingereza: International Fund for Agricultural Development; kifupi: IFAD) ni taasisi ya kifedha ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa yenye jukumu la kushughulikia umaskini na njaa katika nchi zinazoendelea.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

IFAD ilianziswa kama taasisi ya kifedha mnamo mwaka 1977 kupitia azimio la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa 32/107 la tarehe 30 Disemba 1977) kama moja ya matokeo ya Mkutano wa dunia juu ya chakula wa mwaka 1974.

Makao makuu ya taasisi hiyo yapo mjini Roma, Italia, na ni mshirika wa mkutano wa Umoja wa Mataifa ya maendeleo (kwa Kiingereza: United Nations Development Group). [1]

Rais wa IFAD ni Gilbert F. Hounbo kutoka Togo, ambaye alichaguliwa kwa miaka minne tangu 2017.

  1. "UNDG Members". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Mei 2011. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2012.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]