Mfereji wa Bristol


Mfereji wa Bristol (kwa Kiwelisi: Môr Hafren, tafsiri halisi: "Bahari ya Severn") ni ghuba kuu katika kisiwa cha Britania, inayotenganisha Kusini mwa Wales (kutoka Pembrokeshire hadi Bonde la Glamorgan) na Kusini Magharibi mwa Uingereza (kutoka Devon, Somerset hadi Kaskazini mwa Somerset). Inaanzia kutoka kwenye ghuba ndogo ya Mto Severn (kwa Kiwelisi: Afon Hafren) hadi Bahari ya Atlantiki ya Kaskazini. Mfereji huu unapata jina lake kutoka kwa mji na bandari ya Bristol nchini Uingereza.
Sehemu ndefu za pwani zote mbili za mfereji huu zimepewa hadhi ya "Heritage Coast" (Pwani ya Urithi). Maeneo haya yanajumuisha Exmoor, Bideford Bay, rasi ya Hartland Point, Kisiwa cha Lundy, Glamorgan, Rasi ya Gower, Carmarthenshire, Kusini mwa Pembrokeshire na Kisiwa cha Caldey.
Hadi enzi za Tudor, Mfereji wa Bristol ulijulikana kama Bahari ya Severn, na bado unajulikana kwa jina hili katika Kiwelshi: Môr Hafren na Kikornwali: Mor Havren.[1]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Mwanajiografia wa karne ya kumi na sita, Roger Barlow, alielezea eneo la maji linalojulikana kama "Severn Sea" kuwa ni sehemu yote ya bahari iliyo mashariki mwa Visiwa vya Scilly, kati ya Wales na England: E. G. R. Taylor (mhariri), A Brief Summe of Geographie, na Roger Barlow (Abingdon, 2016), uk. 32
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mfereji wa Bristol kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |