Nenda kwa yaliyomo

Omri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mfalme Omri)
Mfalme Omri alivyochorwa mwaka 1553.

Omri (kwa Kiebrania עָמְרִי, ‘Omrī[1]), labda wa kabila la Isakari[2], alikuwa kamanda wa mfalme Ela, akatawala kwa miaka 12 Ufalme wa Israeli baada ya kushindana miaka 4 na Tibni [3]. Ndiye mwanzilishi wa mji wa Samaria[4].

Biblia inamhukumu hasa kwa kuendeleza sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi.

Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Kwanza cha Wafalme, 16.

  1. Thiel, W., "Omri", The Anchor Bible Dictionary, p. 17, vol. 5, D.N. Freedman (ed.). New York: Doubleday (1992)
  2. A History of Ancient Israel and Judah. James Maxwell Miller, John Haralson Hayes. 2006. uk. 266. ISBN 9780664212629. Iliwekwa mnamo 25 Januari 2015.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257
  4. Singer, Isidore; Adler, Cyrus (1905). The Jewish Encyclopedia. Funk & Wagnalls. uk. 401.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Omri kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.